VIGOGO WA CCM WAPATA SHAHADA CHUO KIKUU HURIA
Mkuu
wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT), Dk. Asha-Rose Migiro,
akimpongeza Kada wa CCM, Asha Abdallah Juma, baada ya kumtunuku shahada
ya pili ya Biashara ya Chuo hicho, katika mahafali ya 25, yaliyofanyika
leo, Makao Makuu ya OUT, Bungo, Kibaha mkoa wa Pwani. Kushoto ni Makamnu
Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Tolly Mbwette. Asha ambaye sasa ni Mjumbe
wa NEC CCM, amewahi kuwa Wazirikatika serikali ya Mapinduzi Zanzibar na
pia Katibu wa NEC, Oganaizesheni.
MKUU
wa Kitengo cha Mawasiliano ya Umma katika Idara ya Itikadi na Uenezi
CCM, Makao Makuu, Daniel Chongolo, akipongezana na Mjumbe wa NEC ya CCM,
Asha Abdallah Juma baada ya wote kutuniwa shahada zao katika mahafali
ya 25 ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT), yaliyofanyika jana, Oktoba
27, Bungo, Kibaha mkoa wa Pwani. Chongolo ametunukiwa shahada ya
kwanza ya Mawasiliano ya Umma na Asha shahada ya Pili ya Biashara.
Katikati ni Kada wa CCM, Rachel Kyala ambaye pia ametunukiwa shahada ya
Mawasiliano ya umma.
Reviewed by crispaseve
on
23:54
Rating:
Post a Comment