Exclusive: Story hii ya Dudu Baya ni fundisho kwa wenye tabia ya kukwepa kupokea simu hasa za wadeni wao, inasikitisha
Exclusive: Story hii ya Dudu Baya ni fundisho kwa wenye tabia ya kukwepa kupokea simu hasa za wadeni wao, inasikitisha
posted 1 day ago by admin
Ni mapema sana ila inabidi niiweke kama alivyonisimuliwa mwenyewe Dudu Baya a.k.a Mamba.
Ni hivi, Dudu Baya alikuwa na mdeni wake wa siku nyingi ambaye
aligeuka kuwa mdeni sugu hivyo alikuwa anamkwepa kwa kuwa alikuwa
anamsumbua mara kwa mara.
Siku moja mwimbaji huyo wa ‘Matope’ alikuwa katika safari zake na
gari lake, mara ghafla akafika eneo ambalo kulikuwa kumetokea ajali
mbaya ya gari na watu wakawa wanafanya kila njia ili waweze kuwaokoa
abiria waliokuwa pale, kwa moyo wa huruma Dudu alijiunga nao katika
zoezi hilo.
“Nilipofika pale nikaona mke wa yule jamaa yangu ninaemdai akiwa na
mtoto wake wanavuja sana damu masikini, ilinisikitisha sana nikaamua
kuwasaidia lakini hali yao ilikuwa mbaya sana.
“Sasa nikampigia simu yule jamaa mdeni wangu nimwambie kilichotokea
huku, jamaa akanichunia hataki kabisa kupokea simu yangu anadhani nataka
kumdai lile deni. Nikapiga simu mara nyingi sana lakini hakupokea.”
Ameeleza Dudu Baya.
Dudu amesimulia kuwa baada ya kufanya taratibu zote na kuwafikisha
hospitalini, bahati mbaya mke na mtoto wakapoteza maisha. Baadae sana,
ndio jamaa akapokea simu aliyopigiwa na Dudu kiasi cha kumaliza chaji ya
kimeo cha mtoto wa Mwanza, na alipopokea tu alianza na maneno
yanayoashiria kuchoshwa na usumbufu wa Dudu.
“Eti baada ya familia yake kupoteza maisha ndo anapokea simu halafu
ananimaindi kuwa namsumbua wakati ameshaniahidi tarehe ya kunipa..aah,
si ndo nikamwambia tukio lenyewe mara akaanza kulia, na kumbe alikuwa
kwenye starehe tu anakula bata.” Ameeleza Dudu.
Tutaimalizia story yote wimbo ukishatoka na video kabisa. Duh, hivi
nilikuwa sijasema kama ni wimbo wake unaotarajiwa kutoka mwaka huu
mwishoni au mwanzo wa mwaka ujao!
Wimbo unaitwa ‘Pokea Simu’ na umepikwa ndani ya Golf Records ilikofanyika 'Matope'.
Dudu ameiambia tovuti hii exclusively kuwa aliamua kufanya wimbo huu
kwa mtindo wa story ya majonzi ili kutoa fundisho kwa watu wenye tabia
za kupotezea simu wanazopigiwa kwa hisia zao binafsi.
Exclusive: Story hii ya Dudu Baya ni fundisho kwa wenye tabia ya kukwepa kupokea simu hasa za wadeni wao, inasikitisha
Reviewed by crispaseve
on
12:24
Rating:
Post a Comment