MAITI YAKUTWA NA KETE 65 ZA DAW ZA KULEVYA
Kete inayosadikika kumuua kijana huyo baada ya kupasukia tumboni.
Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya, Diwani
Athumani, akitoa taarifa kwa waandishi wa habari nje ya ofisi yake huku
akiwa na baadhi ya askari wa jeshi hilo mkoani hapa.
Pasi ya kusafiria kijana huyo alizokutwa nazo...
Kete zilizokutwa tumboni mwa kijana huyo baada ya kufan yiwa upasuaji katika hospitali ya Rufaa ya Mbeya.
Kulia ni kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya, Diwani Athumani, akiwa amevalia mavazi maalum, kwenye chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya rufaa ya Mbeya kwa ajili ya kuona maiti hiyo.
Maiti ya kijana Kassim Said Mboya ukiwa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya rufaa ya Mbeya baada ya kufanyiwa upasuaji na kutolewa dawa zinazodhaniwa kuwa ni za kulevya.
Kete zilizokutwa tumboni mwa kijana huyo baada ya kufan yiwa upasuaji katika hospitali ya Rufaa ya Mbeya.
Kulia ni kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya, Diwani Athumani, akiwa amevalia mavazi maalum, kwenye chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya rufaa ya Mbeya kwa ajili ya kuona maiti hiyo.
Maiti ya kijana Kassim Said Mboya ukiwa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya rufaa ya Mbeya baada ya kufanyiwa upasuaji na kutolewa dawa zinazodhaniwa kuwa ni za kulevya.
*Wananachi
watakiwa kufika Rufaa Mbeya kuitambua
*Ni maiti ya
tatu kukamatwa ikiwa na kete za namna hiyo
Na Gordon
Kalulunga, Mbeya
MAITI ya
kijana Kassim Said Mboya(36), mkazi wa Jijini Dar es Salaam, imekutwa na kete
65 za zinazodhaniwa kuwa ni dawa za kulevya.
Taarifa
zilizolifikia Tanzania daima tangu jana jioni, zilieleza kuwa maiti ya kijana
huyo, ilikutwa katika basi la kampuni ya Taqwa eneo la Kasulumu lililokuwa
likitokea Jijini Dar es Salaam nchini Tanzania na kuelekea nchini Malawi.
kalulunga blog ilifuatilia na kujua ukweli wake kisha kuwasiliana na kamanda wa polisi
mkoa wa Mbeya, Diwani Athumani leo asubuhi, ambaye pia alikiri kuwepo kwa
maiti hiyo na kumwambia mwandishi wakutane eneo la chumba cha maiti cha
hospitali ya Rufaa ya Mbeya kwa ajili ya kuona mwili wa marehemu huyo.
Kamanda wa
polisi wa mkoa wa Mbeya, Diwani Athumani, alisema kuwa kijana huyo kabla
hajafariki, alikamatwa Novemba 7, mwaka huu akiwa ndani ya basi hilo lenye
namba za usajili T 319 BLZ akiwa na tiketi yenye jina la Kassim Mueck Michael.
‘’Awali basi
hilo kabla ya kufika mpakani Kasumulu na abiria kushuka na kuanza kufanya
taratibu za kuvuka mpaka na kuingia nchini Malawi, marehemu alibaki kwenye gari
huku afya yake ikizidi kudhoofika’’ alisema Kamanda Dwani Athumani.
Alisema baada
ya kuona hivyo, wahusika wa basi hilo walitoa taarifa kituo cha polisi ambapo
kijana huyo alichukuliwa na kupelekwa katika hospitali ya wilaya ya Kyela na
kabla hajapata matibabu alifariki dunia.
Alieleza kuwa,
kwa kuwa kijana huyo kabla hajapasuka alikuwa na dalili zilizogundulika kuwa
alikuwa na dawa za kulevya, iliamuliwa mwili huo kusafirishwa mpaka hospitali
ya Rufaa ya Mbeya ambako ulipasuliwa na kukutwa na pipi 65 zinazodhaniwa kuwa
ni dawa za kulevya na moja ikiwa imepasuka.
‘’Natoa rai
kwa wananchi wa mkoa wa Mbeya nan chi nzima kwa ujumla kufika hospitali ya
rufaa ya Mbeya kwa ajili ya utambuzi wa mwili wa marehemu na kwamba ijulikane
kuwa usafirishaji na utumiaji wa dawa za kulevya ni hatari kwa afya ya mtumiaji’’
alisema Kamanda Diwani.
Alipoulizwa kuwa
kutokana na mkanganyiko uliowahi kujitokeza katika upotevu na kuwa dawa
zilizowahi kukamatwa awali hazikuwa dawa, alisema kuwa kikosi kazi chake
kimejipanga vema na jitihada za kupeleka kwa mkemia mkuu zinafanywa chini ya
kikosi kidogo cha ulinzi na usalama cha mpaka wa Kasumulu.
Hii ni maiti
ya tatu kukamatwa na dawa zinazodhaniwa kuwa ni za kulevya mkoani Mbeya, ambapo
shehena ya kwanza ya dawa hizo ilikamatwa mwaka mjini Tunduma mkoani hapa mwaka
2006 ikiwa kwenye tumbo la marehemu Kombo Siriri.
Shehena ya
pili ya dawa hizo ilikamatwa Desemba 5, 2011 katika hotel ya High Class mjini
Tunduma, ikiwa katika tumbo la maiti ya Mshanga Mwasala.
Licha ya
ukamataji wa dawa hizo na baadhi ya watuhumiwa wakiwa haia, hakuna mtuhumiwa
aliyewahi kupatikana na hatia tangu mfululizo wa ukamata dawa hizo zinazodhaniwa
kuwa ni dawa za kulevya mkoani Mbeya.
MAITI YAKUTWA NA KETE 65 ZA DAW ZA KULEVYA
Reviewed by crispaseve
on
12:20
Rating:
Post a Comment