ARSENAL HOI KWA BAYERN
Wojciech Szczesny akijaribu kumzuia Arjen Robben bila mafanikio.
TIMU
ya Arsenal FC imepokea kipigo cha bao 2-0 kutoka kwa Bayern Munich
katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya iliyochezwa Uwanja wa Emirates,
London hivi punde.
Arsenal
waliokuwa nyumbani katika Uwanja wao wa Emirates wamemaliza mchezo
wakiwa 10 baada ya kipa wao Wojciech Szczesny kumchezea rafu wimba wa
Bayern Munich, Arjen Robben aliyekuwa anaelekea kufunga bao.
Baada ya rafu hiyo, Szczesny alizawadiwa kadi nyekundu na kuamriwa ipigwe penalti langoni mwa Arsenal japo David Alaba aliikosa.
Mechi ya leo imeshuhudia timu zote mbili zikikosa penalti ambapo ya Arsenal imekoswa na Mesut Ozil na ya Munich ikikoswa na David Alaba.
Wafungaji mabao ya Munich walikuwa Toni Kroos na Tomas Muller.
(PICHA ZOTE KWA HISANI YA MAIL ONLINE)
ARSENAL HOI KWA BAYERN
Reviewed by crispaseve
on
08:17
Rating:








Post a Comment