HONEY KAUR MAIR AIBUKA MSHINDI WA SHINDANO LA VALENTINES DAY SPECIAL LILILOANDALIWA NA MeTL KWENYE UKURASA WAKE WA FACEBOOK

Honey akiwa amepozi pembeni ya kikapu maalum cha wapendanao, kilichosheheni zawadi mbali mbali.
Na.Mwandishi wetu
Honey
Kaur Mair, ni msichana mwenye bahati. Bila shaka sikukuu yake ya
wapendanao ilimalizika kwa furaha baada ya yeye na mumewe kuibuka
kidedea wa shindano lililoandaliwa na kudhaminiwa na METL la Valentines
Day Special Competition kupitia ukurasa wao wa Facebook. Pamoja na
kuzawadia kikapu maalum cha wapendanao kilichosheheni zawadi kem kem,
pia wapenzi hawa walipatiwa vocha maalum iliyowawezesha kupata dinner
matata usiku wa siku ya Wapendanao katika mgahawa maarufu wa AK's Cafe.
Shindano
hilo lililoshika kasi kuanzia tarehe 5 February na kumalizika tarehe 12
February, lilishuhudia washiriki wengi wakijitosa kuwania zawadi maalum
iliyoandaliwa kwa kutuma picha za couple zao na wapenzi au watu wao
wawapendao ambao wangesherehekea pamoja sikukuu ya wapendanao na picha
zao kuwekwa kwenye ukurasa wa Facebook wa METL kisha kupigiwa kura.
Hatimaye
baada ya mchuano mkali, Honey na mpenzi wake Davinder waliibuka kidedea
kwa kushinda baada ya picha yao kupata LIKES nyingi kushinda wengine
hivyo kumaanisha kwamba wao ndio wamechaguliwa na wengi kama 'best
couple' kushinda shindano hilo.
METL
inapenda kuwapongeza Honey na Davinder kwa ushindi huo na pia
inawashukuru wateja wake wote ambao walishiriki kwa moyo katika shindano
hilo. Kwetu sisi, nyote ni washindi, na hawa ni wawakilishi wenu tu
katika kuchukua zawadi!
ASANTENI, ENDELEENI KUPENDANA KILA SIKU!
Like Ukurasa wetu wa Facebook hapa www.facebook.com/MeTLGroup
HONEY KAUR MAIR AIBUKA MSHINDI WA SHINDANO LA VALENTINES DAY SPECIAL LILILOANDALIWA NA MeTL KWENYE UKURASA WAKE WA FACEBOOK
Reviewed by crispaseve
on
08:15
Rating:



Post a Comment