JAJI MKUU WA ZANZIBAR AFANYA MKUTANO NA WANDISHI WA HABARI.
aji
Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu akizungumza na waandishi wa habari
juu ya sherehe ya siku ya sheria Zanzibar ambayo itaadhimishwa tarehe
10 Februari 2014. Mkutano huo ulifanyika Ofisini kwake Vuga, Mjini
Zanzibar.
Mwandishi
wa habari wa Idara ya Habari Maelezo Ramadhani Ali akimuuliza swali
Jaji Mkuu wa Zanzibar (hayupo pichani) wakati wa mkutano wake na
waandishi wa habari.
Jaji
Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu akitoa ufafunuzi wa jambo wakati
wa mazungumzo yake na waandishi wa habari yaliyofanyika ofisini kwake
Vuga mjini Zanzibar.
Baadhi
ya watendaji wa Mahakama ya Vuga mjini Zanzibar na waandishi wa habari
wakimsikiliza Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu (hayupo pichani)
wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika ofisini kwake
Vuga, Mjini Zanzibar leo. (Picha na Makame Mshenga wa Maelezo Zanzibar).
======== ===== ======
Na Miza Othman Maelezo Zanzibar 31/1/2014
Jaji
Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu amesema ucheleweshwaji wa kesi
katika Mahakama za Zanzibar unasababishwa na mambo mengi ikiwemo
kukosekana mashahidi na kutokamilika kwa upelelezi na ukosefu wa
vitendea kazi.
Hayo
ameyaeleza leo huko Ofisini kwake Vuga wakati alipokuwa akizungumza
na waaandishi wa Habari juu ya sherehe ya siku ya sheria Zanzibar ambayo
itaadhimishwa tarehe 10 Februari 2014.
Amesema
kaulimbiu ya maadhimisho hayo mwaka huu ni “Saidia mahaka kutenda haki
“ ikiwa na lengo wadau wote wa mahakama kutoa mchango wao kuiwezesha
mahakama kutenda haki.
“Kesi
sio mahakama pekee wadau wengi wanahusika na kila mmoja anapaswa
kutekeleza wajibu wake katika utolewaji wa haki lakini inayolaumiwa
zaidi ni Mahakama kwa sababu utoaji wa haki unamalizia hapa” alisema
Jaji Mkuu.
Amesema
kesi za jinai mara nyingi huanzia Polisi na baadae kupelekwa kwa
Mkurugenzi wa Mshtaka na hatimae kuwasilishwa mahakamani kwa mashtaka
lakini mahakama hushindwa kumaliza kesi kwa haraka kutokana na
kukosekana mashahidi na kutokamilika upelelezi.
Kwa
upande wa kesi za madai Jaji Mkuu amesema zimekuwa na changamoto
nyingi baadhi ya wakati mdaiwa hajulikani alipo na mdai anashindwa
kuwa na mawasiliano naye.
Jaji
mkuu wa Zanzibar ameongeza kuwa baadhi ya wakati bajeti nayo inakuwa ni
kikwazo kwani imekuwa haitoshi na haipatikani kwa wakati.
Amesema
siku ya sheria Zanzibar itatoa nafasi kwa wadau wa mahakama ikiwemo
Polisi Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka na serikali kukaa pamoja
kutafakari njia zilizobora za kuendesha kesi kwa haraka.
Akizungumzia
malalamiko ya rushwa katika mahakama, amesema suala hilo linachangamoto
nyingi kwani rushwa hutolewa kwa njia ya siri lakini amewashauri
wananchi wanaoombwa rushwa kutoa taarifa kwa Mamlaka ya Kuzuia Rushwa
kwa hatua zaidi.
Hata
hivyo amekumbusha kuwa suala la rushwa ni kosa linalowahusu mtoaji na
mpokeaji hivyo amewataka wananchi kutokuwa tayari wanapoombwa rushwa
ili kuepuka kuingia kwenye makosa.
Jaji
Makungu amesema kabla ya kilele cha sherehe hiyo kutakuwa na harakati
mbali mbali ikiwemo mdahalo wa wanafunzi utakaozungumzia umuhimu wa
heria na vipindi vya Televisheni na Radio ambavyo vitahusu juu ya siku
hiyo.
JAJI MKUU WA ZANZIBAR AFANYA MKUTANO NA WANDISHI WA HABARI.
Reviewed by crispaseve
on
00:01
Rating:
Post a Comment