Semsekwa katika picha ya pozi.
Banza Stone mmoja wa vivutio katika uzinduzi huo wa kesho.
--
HAYAWI hayawi, sasa yamekuwa! Ule uzinduzi wa albamu ya ‘Mtendwa Akitendewa’ kutoka bendi ya Extra Bongo kesho utafikia kilele ambapo watadondosha bonge la shoo katika ukumbi wa Dar Live, Mbagala-Zakhem.
Akizungumzia
maandalizi ya mwisho kuelekea shoo ya albamu hiyo katika hoteli maarufu
ya Atriums iliyoko Afrika Sana, Sinza, jijini Dar es Salaam,
Mkurugenzi wa Extra Bongo, Ally Choky, alisema kila kitu kinaenda sawa
na hivi sasa kilichobaki ni kudondosha mashambulizi siku ya kesho usiku.
Burudani
hiyo itanoga zaidi kutokana na kusindikizwa na wakali wa Bongo Fleva
kina Amin na Linah, Makhirikhiri wa Bongo, Bendi ya Mashujaa, TOT Band
chini ya ‘Malkia wa Mipasho’ Khadija Kopa.
Kiingilio kitakuwa ni sh. 6,000 tu.
(HABARI/PICHA: ANDREW CARLOS, GPL)

Post a Comment