'Nipe Samaki nikupe Ngono,' Kenya

Akina mama wamewezeshwa sasa kujikumu kwa kuvua Samaki wenyewe
Katika
ufuo wa bahari ya Ziwa Viktoria kuna biashara inayovuma-dau za uvuvi
zilizotengenezwa kwa mbao zimejaa si haba, asubuhi zimejazwa Samaki wa
Tilapia.
Nyakati
za asubuhi na mchana, wavuvi hukusanyika na kupiga foleni kununua
Samaki; wengi wao wakiwemo wanawake ambao wanatumainia kupata faida;
japo kidogo, katika soko lililo karibu.
Ila, katika sehemu hii ya Kenya, biashara hii haifanywi kwa ubadilishanaji wa pesa kwa Samaki.
Malipo ni ubadilishanaji wa ngono kwa Samaki: wanawake wanauza miili yao kwa matumaini kuwa wataeleka nyumbani na Samaki wengi.
Biashara hii inajulikana kama “ubadilishanaji wa ngono kwa samaki” ama, kwa lugha ya kiluo, inajulikana kama “jaboya”.
Lucy
Odhiambo, 35, anatayarisha ununuzi wake wa mwisho, ambao ataupeleka
sokoni; anawapasua samaki na kuwatoa uchafu wa tumboni. Ni mjane, na
mama wa watoto tano, anasema kuwa wanawake hapa wanalazimika kufanya
wasiyotarajiwa kufanya na jamii.
"Inanilazimu niuuze mwili wangu kwa wavuvi ili nipate samaki kwa sababu sina uwezo wa kujikimu", anaiambia BBC.
"Kawaida,
mimi hulala na wavuvi wawili au watatu kwa juma. Naweza pata magonjwa,
ila sina budi kufanya hivyo. Nina watoto ambao nafaa kuwalipia karo.
Jaboya ni tendo baya mno. "
Ugonjwa
anaouongelea hapa ni ukimwi ambao umeenea sana katika eneo hili. Ripoti
za afya zinadhihirisha kuwa ugonjwa wa Ukinmwi umekithiri katika eneo
hili ukiipiku kwa 15% maradufu ile idadi ya wastani ya nchi. Hii
inatokana na biashara hii ya “ubadilishanaji wa ngono kwa samaki.
'Nipe Samaki nikupe Ngono,' Kenya
Reviewed by crispaseve
on
08:12
Rating:
Post a Comment