PICHA: WAMILIKI WA MAENEO YA BIASHARA WAOMBWA KUTOA KIPAUMBELE KWA WANAWAKE WAJASIRIMALI
Hii
ni moja ya zawadi ya kikombe kwa Chama cha Wajasiriamali Wanawake
Tanzania (TANCFRAFT) walichowahi kupata kwa kuonyesha bidhaa zenye ubora
wa kimataifa.
Mwenyekiti
wa Tancraft, Elihaika Mrema akizungumza na waandishi wa habari umuhimu
wa jumuiya kubwa za wafanyabiashara na pamoja na serikali kuwaunga mkono
wajasirimali wanawake nchini, Kushoto ni Esther Kasenga Msaidizi wa
Katibu, Kulia Mweka hazina wa Chama cha Tancraft, Bi.Louise Judicate na
Wapili kulia ni Katibu wa Tancraft, Bi. Vicky Shayo.
Na Damas Makangale, MOblog Tanzania
WAMILIKI
Wote wa maeneo ya biashara nchini wameombwa kutoa nafasi ya maeneo ya
biashara kwa wajasirimali wanawake ili kumkomboa mwanamke kutoka katika
dimbwi la umaskini na utegemezi. MOblog inaripoti.
Akizungumza
na waandishi wa habari pamoja na wajasirimali wanawake jijini Dar es
Salaam leo mchana, Mwenyekiti wa Tanzania Handcraft Association
(Tancraft), Elihaika Mrema amesema kuwa wanawake wafanyabiashara wadogo
wana matatizo na changamoto kadhaa mojawapo ni maeneo ya kuuzia bidhaa
zao.
Pichani
juu na chini ni Baadhi ya Wajasiriamali Wanawake wakifuatilia hotuba ya
mwenyekiti wa TANCRAFT Bi. Elihaika Mrema alipokuwa akizungumza na
waandishi wa habari katika jengo la Biashara la DAR FREE MARKET lililopo
barabara ya Ali Hassan Mwinyi karibu na Ubalozi wa Kenya nchini.
“hata
kama mjasirimali mwanamke ukimpa mtaji wa biashara na mafunzo
changamoto kubwa ni kupata eneo la kuweza kuuza hiyo bidhaa yake
aliyotengeneza kwa mikono yake mwenyewe,” amesema Mrema
Mwenyekiti,
Mrema amesema kuwa chama cha Tancraft kilianzishwa mwaka 2006 chini ya
usimamizi wa Board of External Trade (BET) na Small industrial
Development Organization (SIDO) na kina wanachama zaidi ya 300 kutoka
mikoa yote Tanzania.
Amesema
kuwa Tancraft ni chama cha wajasirimali wanaotengeneza bidhaa kwa
kutumia mali ghafi za kutoka nchini kama vile nguo za batik, vikapu,
minyaa, vitu vya ufinyanzi,vinyago, shanga, bidhaa za ngozi, chakula na
usindikaji wa aiana zote zikiwemo asali.
“malengo
makuu ya chama yalikuwa ni pamoja na kuwatafutia wanachama wake soko la
pamoja kwa ajili ya kuuzia bidhaa zao,” alilisisitiza Mrema
Amesema
kwamba chama cha wanawake wa wajasirimali kimepata sehemu ya Dar es
Salaam Free Market ambapo wajasirimali wakinamama watapata fursa ya
kufanya biashara zao bila kulipa ushuru kama walivyokuwa katika maeneo
ya Chang’ombe mikono.
Mkurugenzi
Mtendaji wa J & L Enterprises, Bi. Louise Judicate Mushi, akitoa
maelezo ya bidhaa zake za mchai chai za aina mbili black na green tea na
mishumaa, amesema kwamba Green Tea ni mchai chai wa kijani kabisa ambao
umesagwa kwa matumizi bora kwa afya ya binadamu
Amesema
uzuri wa kinywaji hicho unaweza kunywa kikiwa cha moto au baridi, mchai
chai ni dawa ya kushusha sukari, homa, presha, misuli na sumu za
mwilini.
Mkurugenzi
Mtendaji wa J & L Enterprises, Bi. Louise Judicate Mushi
akimuonjesha aina ya chai mmoja wa waandishi wa habari kutoka kituo cha
Channel Ten Bw. Salum Mkambala.
Mjasiriamali
Fatuma Amour kutoka kampuni ya Famour Designer, akizungumzia ubunifu
wake wa mavazi na ujasirimali utengenezaji wa nguo za wakinamama na
wakinababa na Carpet za ngozi, viatu vya ngozi, vikapu na Batiki. Fatuma
amesema alianza biashara miaka karibu 12 iliyopita katika biashara yake
ya vitu vya asili vya kiafrika na changamoto kubwa kwake ni
kujitangaza. Kushoto ni mwandishi wa habari kutoka Mwananchi
Communications, Bi. Maimuna Kubegeya.
Maimuna Kubegeya akiangalia moja ya bidhaa zinazotengenezwa na Mjasiriamali Fatuma Amour kwenye jengo
la Biashara la DAR FREE MARKET lililopo barabara ya Ali Hassan Mwinyi
karibu na Ubalozi wa Kenya nchini ambapo watakuwa hapo kwa muda wa mwaka
mmoja.
Mwandishi
wa kituo cha Televisheni cha ITV, Fatma Almasi, akiangalia moja ya
bidhaa zinazotengenezwa na Batiki. Wa pili kulia ni Mwenyekiti wa
Tancraft, Elihaika Mrema na wa tatu kulia ni Mwandishi wa habari kutoka
kituo cha Televisheni cha Channel Ten Bw. Salum Mkambala.
Baadhi ya Wajasiriamali wa DAR FREE MARKET wakionyesha bidhaa zao. Watanzania tuwaunge mkono wenzetu!
Baadhi
ya Wajasiamali Wanawake Tanzania wakionyesha moja ya kazi za Uchoraji
za Ujasiriamali kwa wageni waalikwa baada ya Chama cha Wanawake
Wajasiriamali Tanzania (TANCRATF) kuandaa mkutano na waandishi wa
habari. Kulia ni Glory Matafu na kushoto ni Jacqueline Polycarp.
Picha
hii inauzwa Shilingi Milioni 1.2 inapatikana kwenye Jengo la Biashara
la DAR FREE MARKET lililopo barabara ya Ali Hassan Mwinyi karibu na
Ubalozi wa Kenya nchini ambapo wajasiriamali hao wanafanya biashara zao
hapo kwa muda wa mwaka mmoja.
Fatuma Amour kutoka kampuni ya Famour Designer akionyesha moja ya kazi za mikono yake.
PICHA: WAMILIKI WA MAENEO YA BIASHARA WAOMBWA KUTOA KIPAUMBELE KWA WANAWAKE WAJASIRIMALI
Reviewed by crispaseve
on
23:58
Rating:
Post a Comment