KIVULINI WAADHIMISHA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI JIJINI MWANZA KWA MDAHALO KUHUSU USAWA WA KIJINSIA UNAVYOWEZA KUWA CHACHU YA MAENDELEO KWA JAMII
Mkurugenzi
wa Taasisi ya KIVULINI Bw. Ramadhan Masele kizungumza na wananchi
kutoka jijini Mwanza juu ya umuhimu wa usawa wa kijinsia katika jamii
wakati wa mdahalo wa maadhimisho ya kilele cha siku ya wanawake duniani.
Muasisi
wa asasi isiyo ya kiserikali ya KIVULINI Bi. Maimuna Kanyamala akieleza
jambo wakati wa mdahalo wa wazi kwa wakazi wa jiji la Mwanza katika
kuchochea usawa wa kijinsia kuleta mabadiliko katika jamii. Bi Maimuna
aligusia swala zima la wanawake kuzichangamkia fursa zilizopo hasa swala
la kugombea nafasi mbalimbali za uongozi katika jamii katika harakati
za kuleta mabadiliko.
Bi.
Joyce Kiria mtangazaji na muongozaji wa kipindi cha kutetea haki za
Wanawake, Wanawake Live kinachorushwa na kituo cha EATV akielezea jinsi
waandishi wa habari wanavyoweza kuleta chachu za mabadiliko katika jamii
kwa kutumia taaluma yao. Bi Joyce alisema kwamba waandishi wanapaswa
kutumia weledi wao katika kueleza jamii umuhimu wa kuleta usawa wa
kijinsia.
Ujumbe toka kwa Mkurugenzi wa KIVULINI Bw. Ramadhani Masele. “Chochea Mabadiliko Kuleta Usawa wa Kijinsia”.
KIVULINI
WAADHIMISHA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI JIJINI MWANZA KWA MDAHALO KUHUSU
USAWA WA KIJINSIA UNAVYOWEZA KUWA CHACHU YA MAENDELEO KWA JAMII
Taasisi
inayojishughulisha na utetezi wa haki za wanawake na watoto wa kike
inayojulikana kama KIVULINI ya jijini Mwanza imefanya semina kwa wakazi
wa jiji la Mwanza na vitongoji vyake katika kuadhimisha siku ya wanawake
duniani iliyoadhimishwa hapo jana ulimwenguni kote.
Mdahalo
huo uliyofanyika katika ukumbi wa Nyanza uliopo katikati ya jiji la
Mwanza ilikuwa na lengo la kuelimisha jamii juu ya swala zima la
kuzingatia usawa wa kijinsia ili uweze kuwa chachu ya maendeleo katika
jamii husika. Mdahalo huo ulihudhuriwa na wageni mbalimbali toka ndani
na nje ya jiji la Mwanza.
Mdahalo
huo wa wazi ulikuwa na ujumbe maalum kwa kuelekeza majadiliano ya jinsi
ya kuthamini mchango wa wanawake ili kuleta chachu ya maendeleo katika
jamii. Huku ukiongozwa na kauli mbiu ya “Chochea Mabadiliko Kuleta Usawa
wa Kijinsia.
KIVULINI WAADHIMISHA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI JIJINI MWANZA KWA MDAHALO KUHUSU USAWA WA KIJINSIA UNAVYOWEZA KUWA CHACHU YA MAENDELEO KWA JAMII
Reviewed by crispaseve
on
15:16
Rating:
Post a Comment