Muungano wa Tanzania ni kielelezo cha maendeleo.
Baadhi
ya waandishi wa habari wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa
Rais( Muungano) Samia Suluhu Hassan leo mjini Dodoma.
(PICHA NA HASSAN SILAYO)
|
Na Jovina Bujulu
Muungano wa Tanzania umeendelea kuwa nyenzo na utambulisho muhimu katika kuleta umoja na maendeleo katika taifa.
Hayo
yamesemwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano) Mh.
Samia Suluhu Hassan wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo mjini
Dodoma.
“Miaka
50 ya Muungano imekuwa ni ya mafanikio makubwa ambayo yamewanufaisha
wananchi katika nyaja mbalimbali kijamii, kiuchumi, na Kisiasa” alisema
Waziri Suluhu.
Waziri
Samia alisema kuwa muungano huo umeendelea kuwa kielelezo imara katika
suala la ulinzi na usalama hali iliyowezesha kuwepo kwa amani na utulivu
nchini.
Katika
suala la haki za binadamu Waziri Samia alisema kuwa suala hilo
limeendelea kupewa kipaumbele ndani ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania ambapo wananchi wameendelea kupata haki zao za msingi kupitia
mahakama za Mwanzo hadi za Juu.
Akifafanua
kuhusu suala la elimu Waziri Samia alibainisha kuwa wanafunzi wenye
sifa Tanzania Bara na Zanzibar wanapatiwa mikopo ili kukidhi gharama za
Masomo, hali iliyosabisha uimarishwaji wa elimu ya juu kwani kuwekuwepo
kwa ongezeko la vyuo vya elimu ya juu kutoka 25 mwaka 2015 hadi 63
vilivyopo sasa.
Aidha
Waziri Samia alisema kuwa Serikali hizi mbili zinashirikiana katika
kubuni na kuibua miradi ya Maendeleo inayofadhiliwa na Serikali kwa
Kushirikiana na Wahisanai wa Maendeleo.
“Serikali
hizi zimekuwa na ushirikiano wa pamoja katika masuala ya mandeleo mfano
Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF III, MACEMP, ASDPL na ASDP kwa ujumla
imekuwa ni chachu kubwa ya Maendeleo ya wananchi katika pande zote za
Muungano” Alisema Waziri Samia.
Waziri
Samia aliongeza kuwa Maadhimisho ya Miaka 50 ya Muungano yalizinduliwa
Zanzibar tarehe 1 Machi na Rais wa Zanzibar Dkt. Ally Mohamed Shein
ambapo nembo ya Muungano ilizinduliwa na sherehe za Muungano zitafanyika
Dar es Salaam.
Kauli mbiu ya Mwaka huu ni “Utanzania wetu ni Muungano wetu, Tuulinde, Tuumarishe na Kuudumisha.”
Muungano wa Tanzania ni kielelezo cha maendeleo.
Reviewed by crispaseve
on
07:10
Rating:
Post a Comment