KAMPENI UCHAGUZI MDOGO JIMBO LA KALENGA,CCM YAZIDI KUIVURUGA CHADEMA,YAMNG`OA MWENYEKITI WAKE.
Wananchi
wa Kijiji cha Kikombwe wakiwa wamekusanyika kwenye mkutano wa kampeni
ya uchaguzi mdogo wa CCM,jimbo la Kalenga ,wakimsikiliza mgombea Ubunge
wa jimbo hilo kupitia chama cha CCM,Ndugu Godfrey Mgimwa akijinadi na
kuwaomba kura kwa ridhaa yao awaongoze kama Mbunge
MWENYEKITI wa Kitongoji cha Lupembelwasenga, Jimbo la Kalenga, Iringa
Vijijini, kwa tiketi ya Chadema, Ezekiel Kibiki akikabidhi kadi ya chama
hicho kwa Mwenyekiti wa CCM Iringa Vijijini Delfina Mtavilalo, baada ya
kutangaza kuhamia CCM katika mkutano wa kampeni za uchaguzi mdogo
katika jimbo hilo, leo katika kata ya Lwamgungwe,Iringa Vijini mapema.
Mgombea
Ubunge wa jimbo la Kalenga kupitia chama cha CCM,Ndugu Godfrey Mgimwa
akijinadi na kuwaomba kura kwa ridhaa ya kuwaongoza kama
Mbunge,Wanakijiji wa Lupembe lwasenga,katika kata ya Lwamgungwe,Iringa
Vijini mapema leo jioni.
Mkutano ukiendelea wa kumnadi mgombea Ubunge kupitia tiketi ya chama cha CCM,katika kijiji cha kijiji cha Kikombwe leo
Aliyewahi
kuwa Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA,ambaye kwa sasa ni Katibu wa CCM mkoa
wa Mtwara, Shaibu Akwilombe akimnadi Godfrey Mgimwa, katika mkutano wa
kampeni za uchaguzi mdogo jimbo la Kalenga, Iringa Vijijini, uliofanyika
katika kijiji cha Kikombwe leo.
Baadhi
ya Wanakijiji wakifuatilia mkutano (CCM) wa kampeni wa chaguzi ndogo wa
jimbo la Kalenga,katika kijiji cha Lupembe lwasenga,katika kata ya
Lwamgungwe,Iringa Vijini mapema leo jioni
Baadhi
ya Wanachama wa CCM wakifuatilia mkutano wa kampeni wa chaguzi ndogo wa
jimbo la Kalenga,katika kijiji cha Lupembe lwasenga,katika kata ya
Lwamgungwe,Iringa Vijini mapema leo jioni
Akina
mama wa kata ya Lwamgungwe,Iringa Vijini mapema wakifuatilia mambo
yaliyokuwa yakijiri kwenye mkutano wa kampeni wa CCM,kwa ajili ya
kumnadi mgombea wao.
Godfrey Mgimwa akinadiwa na kuombewa kura kwa wanakijiji cha kata ya Lwamgungwe,Iringa Vijini mapema leo
Wakiwasili kijiji cha Kikombwe leo kwa ajili ya kampeni
Pichani
wa pilia shoto ni Mgombea Ubunge wa jimbo la Kalenga,Godfrey Mgimwa
akiwasili katika kijiji cha Kikombwe leo,kwa ajili ya mkutano wa
kampeni.
Amekwenda kusikiliza yanayosemwa kwenye mkutano wa kampeni.
Katibu wa CCM mkoa wa Iringa Salum Mtenga akizungumza na waandishi wa
habari leo, katika Ofisi ya CCM ya mkoa huo, kuhusu mambo yanavyoendelea
katika kampeni za uchaguzi mdogo jimbo la Kalenga
KAMPENI UCHAGUZI MDOGO JIMBO LA KALENGA,CCM YAZIDI KUIVURUGA CHADEMA,YAMNG`OA MWENYEKITI WAKE.
Reviewed by crispaseve
on
07:10
Rating:
Post a Comment