Pinda, Mengi, Askofu Gamanywa, Mzee wa Upako wachuana Tamasha la Pasaka
WAZIRI
Mkuu wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania, Mizengo Pinda amechomoza kwenye
zoezi la upigaji kura kuchagua mgeni rasmi katika tamasha hilo
linalotarajia kuanza Aprili 20 hapa Tanzania.
Kwa
mujibu wa Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo,
Abihudi Mang’era sambamba na Waziri Mkuu, wengine wanaofuatia katika
zoezi hilo ni Mkurugenzi wa kampuni za IPP, Dk Reginald Mengi na Askofu
Mkuu wa Taasisi ya WAPO Mission International, Sylvester
Gamanywa, mchungaji wa kanisa la Ufufuo na uzima, Josephat Gwajima,
Mchungaji wa kanisa la Maombezi (GRC), Anthony Lusekelo ‘Mzee wa Upako’
pia wanamfuatia Waziri Mkuu katika zoezi la upigaji kura linaloendelea.
Mang’era anaendelea
kuwakumbusha watanzania namna ya kuwapigia kura waimbaji, mgeni rasmi
na mikoa ambako ukitaka kumpigia mwimbaji andika pasaka acha nafsi kisha
andika jina la mwimbaji unatuma kwenda namba 15327.
Pia
kwa mgeni rasmi andika neno pasaka acha nafasi kisha andika jina la
mgeni rasmi unayetaka kumpigia kura tuma kwenda 15327, wakati mikoa
unaandika pasaka acha nafasi jina la mkoa unaotaka kuupigia kura tuma
kwenda namba 15327 piga kura uwezavyo ili upate mwimbaji na mgeni rasmi
na mkoa unaopenda ili tamasha lifanyike.
Aidha
Mang’era mbali ya viongozi hao wa dini na serikali, pia waimbaji Jescar
BM na Bahati Bukuku ni mojawapo ya waimbaji wanaoonekana kuelekea
kupata nafasi ya kushiriki katika tamasha hilo kwa kuwa na kura nyingi.
Mang’era
alisema mikoa ambayo inaongoza kupigiwa kura nyingi ni pamoja na
Mwanza, Mbeya, Kigoma na Dar es Salaam inapigiwa kura nyingi kwa ajili
ya kufanyika kwa tamasha hilo.
Makamu
Mwenyekiti huyo alisema kampuni ya Msama Promotions ambao ni waandaaji
wa tamasha hilo wanazingatia na kutekeleza yale ambayo yanayotakiwa na
wadau ambao wanachagua wanachopenda.
Pinda, Mengi, Askofu Gamanywa, Mzee wa Upako wachuana Tamasha la Pasaka
Reviewed by crispaseve
on
07:09
Rating:
![Pinda, Mengi, Askofu Gamanywa, Mzee wa Upako wachuana Tamasha la Pasaka](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgVhNxnN3IACJI2ZLPrcKW5fxJxdf2Ax3fhC6FKbJEF6VwOFGvEaiBa4f8rJlY5M-7wznqBM6993ugjebPbU0CgeiwUWJUGo1VuvN8d0tjR8ESJCa2YWOMu_tJtu4BOElldLHfUY3iugF6B/s72-c/IMG_99641.jpg)
Post a Comment