PICHA KUTOKA JESHI LA MAGEREZA NCHINI: KIKAO CHA MAANDALIZI YA MKUTANO MKUU WA WAKUU WA MAGEREZA AFRIKA KITAKACHOFANYIKA MSUMBIJI JULAI 2014 CHAFANYIKA NCHINI AFRIKA KUSINI
Mwenyekiti wa Umoja wa Magereza Afrika, Kaimu Kamishna Jenerali wa
Magereza Nchini Afrika Kusini, Nontsikelelo Jolingana akitoa hoja ya
kufungua rasmi Kikao cha Maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Wakuu wa Magereza
Afrika unaotarajiwa kufanyika Nchini Msumbiji Julai 2014. Kikao hicho
kimefanyika hivi karibuni Mwishoni mwa mwezi Februari, 2014 Nchini
Afrika Kusini na kuhudhuliwa na Nchi Wanachama ikiwemo Tanzania.
Baadhi ya Washiriki wa Kikao toka Nchi Wanachama Barani Afrika
wakifuatilia kwa makini mjadala katika Kikao cha Maandalizi ya Mkutano
Mkuu wa Wakuu wa Magereza Afrika unaotarajiwa kufanyika Nchini Msumbiji
Julai 2014.
Washiriki wa Kikao cha Maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Wakuu wa Magereza
Afrika wakiendelea na majadiliano ya Kikao hicho Jijini Johanesberg,
Afrika Kusini hivi karibuni. Mkutano Mkuu wa Wakuu wa Magereza Afrika
unaotarajiwa kufanyika Nchini Msumbiji Julai 2014.
Baadhi ya Wakuu wa Magereza Afrika wakiwa katika picha ya pamoja mara
baada ya kufunga rasmi Kikao cha Maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Wakuu wa
Magereza wa Afrika unaotarajiwa kufanyika Nchini Msumbiji Julai 2014.
Kikao hicho kimefanyika mwishoni mwa mwezi Februari 2014 Jijini
Johanesberg Afrika Kusini(wa kwanza kushoto mstari wa mbele) ni Kaimu
Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini Afrika Kusini, Nontsikelelo
Jolingana(wa kwanza kushoto mstari wa nyuma) ni Kamishna Jenerali wa
Magereza Nchini Namibia, Raphael Hamunyela( wa pili kulia mstari wa
mbele) ni Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini Msumbiji, Dkt. Eduardo
Mussanhane (wa kwanza kulia mstari wa nyuma) ni Kamishna Jenerali wa
Magereza Nchini Tanzania, John Casmir Minja.
Sekretarieti Kuu ya Umoja wa Vyombo vya Urekebishaji/Magereza Afrika
wakiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Vyombo vya
Urekebishaji/Magereza Afrika mara baada ya kufungwa rasmi kwa Kikao cha
Maandalizi ya Kikao cha Maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Wakuu wa Magereza
unaotarajiwa kufanyika Nchini Msumbiji Julai 2014(wa tatu toka kulia
mstari wa nyuma) ni Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini Tanzania, John
Casmir Minja.Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza
PICHA KUTOKA JESHI LA MAGEREZA NCHINI: KIKAO CHA MAANDALIZI YA MKUTANO MKUU WA WAKUU WA MAGEREZA AFRIKA KITAKACHOFANYIKA MSUMBIJI JULAI 2014 CHAFANYIKA NCHINI AFRIKA KUSINI
Reviewed by crispaseve
on
22:22
Rating:
Post a Comment