Rebecca Malope aja Tamasha la Pasaka
MALKIA
wa muziki wa Injili nchini Afrika Kusini, Rebecca Malope ni miongoni
mwa wasanii watakaotumbuiza kwenye Tamasha la Pasaka mwaka huu.
Taarifa
kwa vyombo vya habari iliyotolewa Dar es Salaam jana na Mwenyekiti wa
Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama ilieleza kuwa msanii
huyo amepata kura nyingi kutoka kwa mashabiki waliompendekeza.
“Tunashukuru
kwamba baada ya mapendekezo ya mashabiki tuliwasiliana na Rebecca
ambaye ameonesha uungwana wa hali ya juu na kutukubalia ombi letu.
“Lakini
pamoja na kukubali ana ratiba ya maonesho sehemu nyingine huko kwao,
hivyo ametuambia hatatumbuiza katika mikoa yote ambayo tamasha
litafanyika mwaka huu, hivyo tutaangalia wapi tumpangie kulingana na
ratiba yake.
“Lakini niwahakikishie
mashabiki wetu kwamba msanii huyo tutakuwa naye na sasa ni suala la
Kamati ya Maandalizi kuona ratiba yake ilivyo na kisha nasi tumuweke
kwenye ratiba yetu ili mashabiki wafurahi,” alisema Msama.
Rebecca
amewahi kutamba na albamu za Saturday Nite (aliyoitoa Januari 1, 2009),
Hlala Nami (Novemba 11, 2003), Siyabonga (Desemba 21, 2000), Free at
Last (Novemba 18, 1997), African Classics (Mei 5, 2009) na Greatest Hits
(Januari 10, 2006).
Wasanii
wengine watakaotumbuiza kwenye tamasha hilo ambao tayari
wameshathibitisha ni Upendo Nkone, John Lissu, Upendo Kilahiro, Rose
Muhando na kwaya ya Kwetu Pazuri wote wa Tanzania.
Rebecca Malope aja Tamasha la Pasaka
Reviewed by crispaseve
on
16:32
Rating:
Post a Comment