Wafanyakazi Airtel wachangisha fedha kwa ajili ya wanawake wanaougua kansa
Wafanyakazi
wanawake wa Airtel wakitoa huduma ya chakula kwa wafanyakazi wenzao
wakati wa tafrija fupi waliyoiandaa kwa dhumuni la kukusanya fedha ili
kuwachangia wagonjwa wa kansa waliopo hospitali ya ocean road jijini Dar
es salaam. jana
Mkurugenzi
mtendaji wa Airtel Tanzania, Bw. Sunil Colaso akichangia fedha kwa
huduma ya Airtel Money kupitia simu wakati wa tafrija fupi iliyoandaliwa
na umoja wa wanawake wa Airtel Tanzania kwa dhumuni la kuwachangia
wanawake wanaosumbuliwa na maradhi ya kansa waliopo hospitali ya ocean
road jijini Dar es salaam.
Mmoja
kati ya wafanyakazi wa Airtel, Bw. Deodatus Hondo akichangia fedha
wakati wa tafrija fupi iliyoandaliwa na umoja wa wanawake wa Airtel
Tanzania kwa dhumuni la kuwachangia wanawake wanaosumbuliwa na maradhi
ya kansa waliopo hospitali ya ocean road jijini Dar es salaam.
======== ======= =======
Wafanyakazi Airtel wachangisha fedha kwa ajili ya wanawake wanaougua kansa
Umoja wa wafanyakazi wanawake wa Airtel Tanzania unaofahamika kwa jina la Airtel Divas leo wameandaa halfa
ya kuchangisha pesa kwa ajili yakina mama wanaosumbuliwa na maradhi ya
kansa katika hospitali ya ocean road jijini Dar es salaam.
Halfa
hiyo ya kuchangisha pesa ilifanyika katika makao makuu ya ofisi za
Airtel Tanzania na kushirikiksha wafanya kazi wa Airtel Tanzania kwa
ujumla
Akizungumza
kwa niaba ya Airtel Ofisa Mahusiano na matukio Dangio Kaniki alisema”
Airtel Tanzania kupitia Umoja wa wanawake Airtel Divas” tumeamua
kuchangisha pesa kwaajili ya kina mama wenzetu ambao ni wagonjwa
mahospitalini, ambapo leo tumeaandaa kifungua kinywa kwa wafanyakazi
wote wa Airtel na kiasi cha pesa kitakachopatikana kitaenda kusaidia
wanawake wanaougua ugonjwa wa kansa katika hospitali ya Ocean Road
jijini Dar es Saalam.
Tunatambua
jamii inayotuzunguka ina changamoto nyingi ikiwemo maradhi, na ndio
sababu umoja wa wanawake wa Airtel tumeamua kuchangisha pesa kwa dhumuni
la kuwasaidia wagonjwa hususani wakina mama wanaosumbuliwa na ugonjwa
kansa. Tunaamini zoezi hili tunalolifanya leo litatuwezesha kufanikisha
lengo letu. Mpango huu wa kusaidia jamii zinazotuzunguka ni endelevu,
na tumejipanga kutoa misaada ili kuchangia katika kutatua vikwazo
mbalimbali vya maisha na kujenga jamii iliyo bora. alisema Kaniki.
Kwa
upande wa wafanyakazi Bi Doris Kibassa ambaye ni mmoja ya wanachama wa
Airtel Diva alisema “ najisikia furaha kuwa sehemu ya kusaidia jamii,
mbali na kampuni yetu kuwa na shughuli za kijamii bado sisi kama
mfanyakazi tunanafasi ya kushiriki na kutoa msaada kwa jamii. Tunaamini
mchango huu tunaoutoa leo utaweza kunusuru maisha ya baadhi ya
watanzania na hivyo basi tunaziasa asasi nyingine kuiga mfano huu na
kushiriki katika kuokoa maisha ya watanzania walio wengi,”
Airtel
Tanzania imekuwa ikitoa michango kwa jamii kutupitia shughuli zake za
huduma kwa jamii, Airtel kwa kushirikisha wafanyakazi wake pia inatoa
huduma kwa jamii nchini.
Wafanyakazi Airtel wachangisha fedha kwa ajili ya wanawake wanaougua kansa
Reviewed by crispaseve
on
16:31
Rating:
Post a Comment