RIDHIWANI AANZA HARAKATI ZA KUSAKA KURA JIMBO LA CHALINZE
Meneja
wa Kampeni za Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze kupitia Chama Cha
Mapinduzi (CCM),Ndg. Steven Kazidi (kushoto) akimuinua mkono juu kwa
ishara ya kumnadi Mgombea Ubunge wa Jimbo hilo (CCM),Ndg. Ridhiwani
Jakaya Kikwete wakati wa mkutano wa kwanza wa kampeni uliofanyika katika
kijiji cha Matipwili,Saadani Wilayani Bagamoyo jana Machi 14,2014.
Mgombea
Ubunge wa Jimbo la Chalinze,Ndg. Ridhiwani Jakaya Kikwete
akinong'onezwa jambo na Mmoja wa kinamama wa Kijiji cha Matipwili (Jina
lake halikuweza fahamika mara moja).
Mgombea
Ubunge wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi ya CCM,Ndg. Ridhiwani Jakaya
Kikwete akiwahutubia wanakijiji wakazi wa Kijiji cha Mkange,Saadani
Wilayani Bagamoyo waliojitokeza kwa wingi kumsikiliza huku wengi
wakiahidi kumpa kura zao pindi itakapofika siku ya Uchaguzi huo mdogo wa
Jimbo hilo.
RIDHIWANI AANZA HARAKATI ZA KUSAKA KURA JIMBO LA CHALINZE
Reviewed by crispaseve
on
09:54
Rating:
Post a Comment