WATANZANIA WAHIMIZWA KUSOMA MAJARIDA MBALIMBALI ILI KUJIONGEZEA UFAHAMU
Baadhi ya Waandishi wa Habari wakifuatilia kwa makini mada mbalimbali na Mafunzo katika semina hiyo
******
Na Arusha yetu Blog
IMEELEZWA kuwa Watanzania ni wavivu wa kusoma Majarida mbali mbali yanayoweza kuwaongezea upeo ukilinganisha na nchi zingine.
Hayo
yamebainishwa na Mmoja wa maafisa wa Jarida la Mkulima Mbunifu,
Caroline Nyakundi kutoka Nchini Kenya, wakati akizungumza katika mafunzo
ya waandishi wa habari za kilimo na wataalamu wa kilimo yanayofanyika
katika ukumbi wa Hoteli ya Arusha Crown ya Mjini hapa.
Ameongeza kuwa kunatofauti kubwa ya Mwitikio wa kusoma machapisho kati ya Raia wa Tanzania ukilinganisha na Kenya ambako imeelezwa kuwa wanauhitaji mkubwa wa kujifunza mbinu mpya za kilimo tofauti na Watanzania ambao hawana uhitaji wa kusoma na kutaka kujua
zaidi.
Akieleza
Mikakati ya Jarida la Mkulima Mbunifu mmoja katika ya Maafisa wa Jarida
hilo, Caroline Nyakundi kutoka Nchini Kenya, amesema tangu kuzinduliwa
kwa jarida hilo Juni,2011 limeonesha mwitikio mkubwa kutokana na kupata
taarifa nyingi kutoka kwa wakulima wakilihitaji ili kujua zaidi habari
za Kilimo.
Amesema Jarida hilo limelenga zaidi maoni na mahitaji ya Mkulima kutokana na mawazo yao ambayo wamekuwa wakiyatoa katika jarida hilo mara kwa mara jambo linaloonesha Mkulima kufikiwa na Jarida hilo na kwa wakati.
WATANZANIA WAHIMIZWA KUSOMA MAJARIDA MBALIMBALI ILI KUJIONGEZEA UFAHAMU
Reviewed by crispaseve
on
07:34
Rating:
Post a Comment