MUNICH, Ujerumani
Arsenal
imeshindwa kufuzu hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada
ya kulazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Bayern Munich, kwenye Uwanja
wa Allianz Arena jijini Munich, jana hivyo kutolewa kwa jumla ya mabao
3-1 kwa kuwa katika mechi ya kwanza Arsenal ilifungwa mabao 2-0.
Mfungaji
wa Bayern alikuwa ni Bastian Schweinsteiger katika dakika ya 54,
Arsenal ikasawazisha kupitia kwa Lukas Podolski katika dakika ya 57 kwa
shuti kali baada ya nahodha wa Bayern, Philipp Lahm kujichanganya.
Mechi
nyingine ya ligi hiyo ilishuhudia Atletico Madrid ikitoa kipigo cha
mabao 4-1 kwa AC Milan, hivyo kusonga mbele kwa jumla ya mabao 5-1,
wafungaji wa Atletico wakiwa ni Diego Costa dakika ya tatu na 85, Arda
Turan (40) na Raúl García (70), huku ikikumbukwa kuwa Milan ilichapwa
bao 1-0 katika mechi ya kwanza.
Bayern Munich: 1-Manuel
Neuer; 21-Philipp Lahm, 4-Dante, 8-Javi Martinez, 27-David Alaba;
6-Thiago Alcantara, 31-Bastian Schweinsteiger; 10-Arjen Robben, 19-Mario Goetze, 7-Franck Ribery; 9-Mario Mandzukic
Substitutes: 22-Tom Starke, 5-Daniel van Buyten, 13-Rafinha, 17-Jerome Boateng, 25-Thomas Mueller, 39-Toni Kroos, 14-Claudio Pizarro
Arsenal: 21-Lukasz
Fabianski; 3-Bacary Sagna, 4-Per Mertesacker, 6-Laurent Koscielny,
5-Thomas Vermaelen; 8-Mikel Arteta, 11-Mesut Ozil, 15-Alex
Oxlaide-Chamberlain; 19-Santi Cazorla, 12-Olivier Giroud, 9-Lukas
Podolski
Substitutes: 13-Emiliano Viviano; 25-Carl Jenkinson, 7-Tomas Rosicky, 20-Mathieu Flamini, 44-Serge Gnabry, 45-Isaac Hayden
Post a Comment