KUMBUKUMBU YA KIFO CHA MANGWEA JUNI 28, SAMAKI SAMAKI MOROGORO
Na Andrew Chale
MASTAA
mbalimbali nchini wakiwemo wanamuziki wanatarajiwa kushiriki kwenye
tukio maalum la kumbukumbu ya mwaka mmoja tokea kifo cha marehemu
Albert Mangwea ‘Ngwair’ , litakalofanyika ndani ya ukumbi wa Nyumbani Park (Samaki samaki Spot) , Kihonda Morogoro mjini Juni 28.
Akizungumza
na mtando huu , Mratibu Mtendaji wa tamasha hilo, Kareeem Omary ‘KO’
alisema maandalizi ya tukio hilo litakalokuwa la kila mwaka, limepwa jina la ‘Love Concert - Kumbukumbu ya kifo cha Albert Mangwe’.
Kareem,
aliwaomba wadau kujitokeza kwa wingi kuunga mkono kwenye tukio hilo
kwani litakuwa la kipekee na la aina yake ambalo pia litatoa fursa kwa
wakazi hao pia mikoa jirani na watu kutoka nje ya Tannzania ambao
watauzulia.
“Nawaomba
wadau kujitokeza kuonesha upendo wa pamoja. Kumbukumbu kwa mpendwa
wetu kama ilivyo utamaduni wetu.” alisema Kareem. Na kuongeza kuwa, siku
hiyo Watu mbalimbali watapata kupiga picha na mastaa pamoja na mama
mzazi wa Mangwea kama kumbukumbu.
Kareem
aliwataja wasanii watakaotoa burundani, ni pamoja na kutoka kwa kundi
la Wanachemba ambalo pia aliwahi kuwa nalo marehemu Ngwair, JSqueezer, P
Funky Majani na Mswaki. Kwa upande wa wasanii kutoka Morogoro ni pamoja
na Afande Sele, Team Racers, Mc Koba Chris wa Marya, Belle 9, Samir,
Zombie, President Mirrow, Jordan wa Dejavu na wengine wengi.
Katika
siku hiyo ya Juni 28, ambayo ndiyo siku aliyopatwa na umati marehemu,
Kareem alisema kabla ya matukio ya shoo ukumbini, itatanguliwa na ibada
mbili maalum ikiwemo ya Kanisani na ile ya nyumbani.
Aidha,
Kareem alisema katika tukio hilo, ambalo linatarajia kuanza majira ya
jioni ya saa 10 hadi saa 12 jioni, wametoa fursa kwa watoto kutoa
burudani ikiwemo ya kuimba na nyinginezo na baadae usiku wa kuanzia saa
2 hadi majogoo wasanii hao mbalimbali watatawala jukwaa na burudani ya
nguvu ya kumbukumbu.
Marehemu ‘Ngwair’ alifariki dunia akiwa nchini Afrika kusini, alijizolea
umaarufu kwa nyimbo kama Mikasi na Nisikilize Mi na nyingine nyingi
alizowahi shirikishwa na wasanii mbalimbali nchini wakiwemo Professa
Jay, Nuru, TID, Chidi Benz na wengine wengi.
KUMBUKUMBU YA KIFO CHA MANGWEA JUNI 28, SAMAKI SAMAKI MOROGORO
Reviewed by crispaseve
on
02:47
Rating:
Post a Comment