MV KIGAMBONI KUSIMAMA KWA MATENGENEZO, MV MAGOGONI NA MV LAMI KUENDELEA NA HUDUMA
Wakala
wa Ufundi na Umeme (Temesa) umetangaza kukipeleka kwenye matengenezo
makubwa kivuko cha Mv Kigamboni, kinachotoa huduma ya kuvusha watu na
magari kwenda na kurudi Kigamboni jijini Dar es salaam.
Aidha
huduma za uvushaji watu pamoja na magari zitaendelea kutolewa na vivuko
vya Mv Magogoni pamoja na Mv Lami katika kipindi chote cha matengenezo
husika.
Ofisa
Habari wa Temesa, Theresia Mwami alimwambia mwandishi jana kuwa wakala
huo unaomba radhi kwa usumbufu ambao wananchi wanaotumia vivuko
watakaoupata wakati kivuko hicho kitakapokuwa kwenye matengenezo.
Mwami
alisema vivuko hivyo havijafanyiwa matengenezo makubwa kwa muda mrefu
hivyo kitafanyiwa matengenezo kivuko cha Mv Kigamboni kwanza na baadae
Mv Magogoni.
Alisema
kivuko cha Mv Lami kina uwezo wa kuchukua abiria 100 na magari madogo
16 wakati kivuko cha Mv Kigamboni kinachukua magari 23 na abiria 800.
MV KIGAMBONI KUSIMAMA KWA MATENGENEZO, MV MAGOGONI NA MV LAMI KUENDELEA NA HUDUMA
Reviewed by crispaseve
on
01:08
Rating:
Post a Comment