Header AD

ZIARA YA KATIBU MKUU WA CCM NDUGU KINANA YAZIDI KUCHANJA MBUGA JIMBO LA BAHI,KESHO KUIVURUGA KONDOA


Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi wa kijiji cha Misisi kata ya Misisi,wilayani Bahi mapema leo,mkoani Dodoma akiwa ziarani ndani ya jimbo la Bahi.

Ndugu Kinana amezungumza na wananchi hao waliokuwa wamebeba mabango na kuzuia msafara wake,kutokana na matatizo yaliyokuwapo katika kijiji hicho na kukosa ufumbuzi kwa muda mrefu.Wananchi hao walikuwa na lalamiko lao moja kubwa lililohusu shule yao ya msingi ya Msisi,ambayo madarasa yake mawili yaliezuliwa paa (kama yaonekanavyo pichani) na mengine kubomoka kabisa kufuatia mvua kubwa ilionyesha na kusababisha madhara hayo.

Shule hiyo ya msingi Msisi ilipatwa na dhahma hiyo mnamo mwaka 2011,na mpaka leo haikuwahi kufanyiwa ukarabati wa aina yoyote huku walimu na wanafunzi wakipigwa na jua wakati wa masomo.Ndugu Kinana baada ya kusikiliza lalamiko hilo kutoka kwa wanakijiji hao,alianzisha harambee ya papo kwa papo iliyohusu viongozi wa CCM mkoa na Wilaya waliokuwa kwenye msafara huo na kuichangia shule hiyo na kufanikiwa kupata fedha na vifaa vya ujenzi ambavyo vitapelekea kuanza upya kwa ujenzi wa madara hayo,Aidha Wananchi wa kijiji hicho walimshukuru Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana kwa harambee alioifanya na kupelekea kupatikana kwa misaada hiyo.

Ndugu Kinana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye wapo kwenye ziara ya siku tisa mkoani Dodoma ya kukagua,kuhimiza na kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2010 pamoja na kusikiliza matatizo ya wananchi na kuyatafutia ufumbuzi.
 Mmoja wa wananchi wa kijiji cha Msisi akiwa amebeba bango lake kichwani.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye akisoma moja ya bango lililokuwa limebebwa na mmoja wa wananchi wa kijiji cha Msisi,Wilaya ya Bahi lililohusu shule ya msingi ya kijiji hicho kukosa madarasa ya kusomea wanafunzi,kufuatia mvua mkubwa kuezua mapaa.
  Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana,Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Mh Chiku Galawa na
 Mbunge wa Jimbo la Bahi,Mh Omari Badwel wakishiriki uchimbaji wa mitaro na kufukia bomba za maji,katika kijiji cha Nguji kata ya Mundemu wilaya ya Bahi mkoani Dodoma.Mradi huo wa maji unatarajiwa kuhudumia zaidi ya watu elfu tatu,aidha mradi huo uliogharimu kiasi cha fedha zaidi ya Milioni mia saba unatarajiwa kukamilika Aprili 15,2015.
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akipokelewa katika kijiji cha Mundemu wilaya ya Bahi mkoani Dodoma 
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizungumza na Wananchi wa Bahi mara baada ya

kumaliza kuzungumza na Halmashauri kuu ya Wilaya ya Bahi,ambapo pia Wananchi waliruhusiwa kuuliza maswa na kupatiwa majibu papo kwa papo.
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akikagua chanzo cha maji (kisima) chenye ujazo wa lita 16 kwa saa,kinachotumia umeme wa jua
 Pichani kushoto ni Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akishiriki kupalilia majani katika
 shamba la mizabibu la Lubala Succoss,katika kata ya Ilindi,wilaya ya Bahi

 Baadhi ya wananchi wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM,Ndgu Kinana alipokuwa
 akizungumza nao jioni ya leo katika kijiji cha kangogo kata ya Babayu,amapo pia alishiriki ujenzi wa nyumba ya waalimu.
 Baaddhi ya Wanahabari wakiwa kwenye mkutano wa hadhara wa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana,uliofanyika katika kijiji cha Chonde,wilaya ya ya Bahi mkoa wa Dodoma.


Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Chonde wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu
 Kinana alipowahutubia jioni ya leo kwenye mkutano wa hadhara,wilayani Bahi mkoa wa Dodoma.
 Wanachi wa kijii cha Chonde wakishangilia wakati Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alipokabidhiwa Mkuki na kuvalishwa mgolole ikiwa ni ishara ya kuwa mmoja wa machifu wa kabila la Wagogo
  Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiendesha trekta ikiwa ni ishara ya kuzindua mradi
wa matrekta katika kijiji cha Chonde,Wilaya ya Bahi mkoani Dodoma jioni ya leo.
  Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye akiendesha trekta,wakati Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alipozindua mradi huo wa matrekta katika kijiji cha Chonde,Wilaya ya Bahi mkoani Dodoma jioni ya leo.
  Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Chonde wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alipowahutubia jioni ya leo kwenye mkutano wa hadhara,wilayani Bahi mkoa wa Dodoma.
ZIARA YA KATIBU MKUU WA CCM NDUGU KINANA YAZIDI KUCHANJA MBUGA JIMBO LA BAHI,KESHO KUIVURUGA KONDOA  ZIARA YA KATIBU MKUU WA CCM NDUGU KINANA YAZIDI KUCHANJA MBUGA JIMBO LA BAHI,KESHO KUIVURUGA KONDOA Reviewed by crispaseve on 02:55 Rating: 5

No comments

Post AD