EU, UN WAFAGILIA JUHUDI ZA KUBORESHA HALI ZA WANAWAKE TANZANIA
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa shirika la
Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akitoa salamu za Umoja wa
Mataifa kwenye maadhimisho ya siku ya kimataifa ya wanawake duniani
ambapo kitaifa ilifanyika mkoani Morogoro miwshoni mwa juma.
Na Modewjiblog team, Morogoro
SERIKALI
ya Tanzania imepongezwa na Umoja wa mataifa kwa juhudi zake kubwa
inazofanya katika kuhakikisha kuna usawa wa jinsia nchini humu.
Kauli
hiyo imetolewa na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na
Mwakilishi wa shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez
wakati alipopewa nafasi ya kuhutubia umati wa watu waliokusanyika
kusherehekea siku ya wanawake duniani ambayo kitaifa ilifanyika
Morogoro.
Alisema
mbele ya Rais Jakaya Kikwete kwamba kazi kubwa iliyofanywa na serikali
ya awamu ya nne ya kutekeleza maazimio ya kimataifa kuhusu usawa wa
jinsia umeifanya Tanzania kuwa moja ya mataifa yanayostahili kupigiwa
mfano.
Akitoa
salamu za Umoja wa Mataifa kutoka kwa Katibu Mkuu Ban Ki Moon, mratibu
huyo alisema kwamba katika bara la Afrika Tanzania imefanya makubwa
katika kuhakikisha usawa wa jinsia na wanawake kuwezeshwa katika masuala
mbalimbali yakiwemo ya kisiasa na utawala.
Balozi
wa Jumuiya ya Ulaya nchini, Filiberto Ceriani Sebregondi akisoma risala
wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya wanawake duniani ambapo
kitaifa ilifanyika mkoani Morogoro.
Alisema
Tanzania imepiga hatua kubwa katika masuala ya usawa kijinsia na
kutolea mfano wa kuwapo kwa asilimia 36 ya wanawake Bungeni.
Aidha
amesema kuanzishwa kwa mifumo inayohakikisha kwamba wanawake wanapata
nafasi sawa katika masuala ya uongozi, elimu na pia kupitishwa kwa
sheria kali ya kukabiliana na masuala ya unyanyasaji na ukatili dhidi ya
wanawake.
Aidha
alisema kwamba miaka 20 iliyopita hali haikuwa sawa lakini kwa sasa
kuna mabadiliko makubwa japo yanatakiwa mengi zaidi ili kukabiliana na
changamoto zilizopo sasa.
Hata
hivyo ameitaka serikali kufanya juhudi zaidi katika kukabiliana na
ukatili dhidi ya wanawake na wasichana na kuhakikisha kwamba wanawake
wanakuwa na sauti katika ngazi zote za utawala kuanzia katika kaya.
EU, UN WAFAGILIA JUHUDI ZA KUBORESHA HALI ZA WANAWAKE TANZANIA
Reviewed by crispaseve
on
02:45
Rating:
Post a Comment