Mamlaka ya Elimu Tanzania inatarajia kukabidhi madawati 2000 kwa shule za Msingi 10
Meneja
Habari, Elimu na Mawasiliano toka Mamlaka ya Elimu Tanzania Bi Sylvia Lupembe
akiongea na waandishi wa habari (Hawapo pichani) kuhusu jitihada wanazofanya
kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ili kukabiliana na changamoto katika sekta
ya elimu,wakati wa mkutano uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Mkuu
wa kitengo cha Masoko na Uhusiano toka benki ya KCB Bi. Christina Manyenye.
Mkuu
wa kitengo cha Masoko na Uhusiano toka benki ya KCB Bi. Christina Manyenye
akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) mipango waliyoiweka kwa
kushirikiana na Mamlaka ya Elimu Tanzania katika kuendeleza na kuinua sekta ya Nchini.kushoto
ni Meneja Sheria na Uhusiano toka kampuni ya uuzaji na usambazaji wa mafuta ya
TOTAL Bi. Masha Msuya.
Afisa
Rasilimali Fedha toka taasisi isiyo ya kiserikali ya Social Action Trust Fund
(SATF) Bw. Timotheo Tenga akiwaeleza jambo waandishi wa habari( hawapo pichani)
wakati wa mkutano uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Meneja Sheria
na Uhusiano toka kampuni ya uuzaji na usambazaji wa mafuta ya TOTAL Bi. Masha
Msuya.
Baadhi
ya waandishi wa habari waliohudhuria mkutano huo wakiwasikiliza wawasilishaji
toka Mamlaka ya Elimu Tanzania, KCB, TOTAL, Social Action Trust Fund (SATF) leo
Jijini Dar es Salaam. PICHA
NA HASSAN SILAYO-MAELEZO.
======= ========
Frank
Mvungi-Maelezo.
Mamlaka
ya Elimu Tanzania inatarajia kukabidhi
madawati 2000 kwa shule za Msingi 10 zilizopo jijini Dara es salaam katika
kukabiliana na Tatizo la upungufu wa madawati hapa nchini. Hayo
yemesemwa na Meneja Habari Elimu na Mawasilano wa Mamlaka ya hiyo Bi Sylvia Lupembe wakati wa mkutano na
waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam.
“Wanafunzi
zaidi ya 6000 watanufaika na madawati hayo ambayo yatagharimu zaidi ya shilingi
Milioni Mia Moja na Hamsini (150,000)” alisema Lupembe. Akifafanua
Bi Lupembe amesema shule zitakazonufaika ni Chamazi, Mbande, Boko NHC, King’ong’o,
Hekima, Bwawani, Bunju, Goba, Kombo na Kingugi.
Katika
kuhamasisha wadau wengine kushiriki kwenye mchakato wa kuchangia madawati Bi
Lupembe amesema kuwa Mamlaka ya Elimu Tanzania imezingatia rai iliyotolewa na
Waziri Mkuu ikielekeza kuwa tatizo la madawati katika shule za msingi
limalizike ifikapo mwezi Juni, 2015 kwa kulipa kipaumbele suala hilo. Pia
Bi Lupembe alibainisha kuwa tathmini ya mwaka 2013 Tanzania ina upungufu wa
madawati 1,147,471 hivyo ni jukumu la kila mdau kuunga mkono juhudi hizo ili
kuondoa tatizo hilo kote nchini.
Naye
Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mahusiano wa benki ya KCB Bi Christina Manyenye
amesema wamekuwa wakishiriki katika kuchangia madawati ambapo kwa mwaka jana walichangia
zaidi ya madawati 700.
“Tutaendelea
kusaidia huduma za jamii katika maeneo mablimbali kama tunavyofanya katika
sekta ya Elimu” alisisitiza Manyenye Mamlaka
ya Elimu Tanzania kwa kushirikiana na Kampuni ya Mafuta ya TOTAL na wadau
wengine kama Kenya Commercial Bank
(KCB), na Social Action Fund wamekuwa
katika ushirikiano tangu mwaka 2013 katika kutatua changamoto mbalimbali
zinazoikabili sekta ya Elimu hapa nchini ikiwemo ya upungufu wa madawati.
Mamlaka ya Elimu Tanzania inatarajia kukabidhi madawati 2000 kwa shule za Msingi 10
Reviewed by crispaseve
on
01:27
Rating:
Post a Comment