RAIS KIKWETE AWEKA JIWE LA MSINGI LA UJENZI WA DARAJA LA KILOMBERO
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe baada ya kuweka jiwe la
msingi la ujenzi wa daraja la kudumu juu ya mto Kilombero wilayani
Kilombero mkoa wa Morogoro Agosti 20, 2014.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akishangiliwa baada ya kuweka jiwe la msingi
la ujenzi wa daraja la kudumu juu ya mto Kilombero Agosti 20, 2014.
Pamoja naye ni Waziri wa Ujenzi Dkt John Pombe Magufuri (kushoto kwa
Rais), Waziri wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Mbunge
wa Ulanga Mashariki Mhe. Celina Kombani (kulia), Mbunge wa Mama Salma
Kikwete (nyuma ya Rais), Mbunge wa Ulanga Magharibi Dkt Haji Ponda
(kulia) na Mbunge wa Kilombero Mhe Abdul Mteketa (kulia kwa Rais)
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo toka Mtendaji Mkuu wa Wakala
wa Barabara (TANROADS) Bw. Patrick Mfugale juu ya ujenzi wa daraja la
kudumu juu ya mto Kilombero Agosti 20, 2014. Kushoto ni Waziri wa
Ujenzi Dkt John Pombe, Magufuri akifuatiwa na Mama Salma Kikwete.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipungia wananchi kwa furaha wakati
akielekea ukingoni mwa Mto Kilombero kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa
daraja la kudumu juu ya mto Kilombero Agosti 20, 2014. Anaoongozana nao
ni pamoja na Waziri wa Ujenzi Dkt John Pombe Magufuri (kushoto kwa
Rais), Waziri wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Mbunge
wa Ulanga Mashariki Mhe. Celina Kombani (kulia), Mkuu wa Mkoa wa
Morogoro Mhe. Joel Bendera (kushoto) na Mama Salma Kikwete (nyuma ya
Rais).
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wananchi baada ya kuweka jiwe la
msingi la ujenzi wa daraja la kudumu juu ya mto Kilombero wilayani
Kilombero mkoa wa Morogoro Agosti 20, 2014
Magari yakivuka juu ya daraja la muda la Mto Kilombero lililojengwa
kurahisisha kazi za ujenzi wa daraja la kudumu katika wilaya ya
Kilombero Mkoa wa Morogoro, wakati wa sherehe za uwekaji jiwe la msingi
wa ujenzi wa darajan hilo na Rais Jakaya Mrisho Kikwete Agosti 20,
2014.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akijaribu madawati mapya ya shule ya
msingi ya Epauko wilayani Mahenge baada ya shule hiyo kukabidhiwa msaada
wa madawati 500 na Kampuni ya Kibaran Resources Ltd inayojishughulisha
na uchimbaji wa madini aina ya Graphite na Nickel mkoani wa Morogoro
Agosti 20, 2014.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete na mmoja wa
wanafunzi wa shule ya msingi ya Epauko wilayani Mahenge baada ya shule
hiyo kukabidhiwa msaada wa madawati 500 na Kampuni ya Kibaran Resources
Ltd inayojishughulisha na uchimbaji wa madini aina ya Graphite na Nickel
mkoani Morogoro Agosti 20, 2014.PICHA NA IKULU
RAIS KIKWETE AWEKA JIWE LA MSINGI LA UJENZI WA DARAJA LA KILOMBERO
Reviewed by crispaseve
on
01:39
Rating:
Post a Comment