Diamond Motors wazindua gari jipya la Mitsubishi 2015 ASX jijini Dar es Salaam
Wema Sepetu akiwasha gari Jipya la ASX Mitsubishi katika uzinduzi wa gari hilo jijini Dar es Salaam.
Hili ndilo gari la ASX Mitsubish jipya lililozinduliwa wiki iliyopita katika hoteli ya serena jijini Dar es Salaam
Millard Ayo, Wema wasifia gari jipya la 2015 Mitsubishi ASX.
Mtangazaji
wa Clouds FM, Millard Ayo na mwigizaji maarufu nchini, Wema Sepetu wamesifia gari
jipya la Mitsubishi ASX la mwaka 2015 linalouzwa na kusambazwa na kampuni ya
Diamond Motors (Hansa Group).
Katika
uzinduzi wa kutambulisha gari hilo uliofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es
Salaam, pamoja na mambo mengine Kampuni ya Diamond Motors wauzaji pekee wa
magari kutoka Mitsubishi waliwaalika Millard Ayo na Wema Sepetu kujaribu gari
hilo toleo jipya Mitsubishi ASX kabla ya uzinduzi.
Mastaa
hao walivutiwa na mwonekano wa Mitsubishi ASX lenye vioo vya kisasa juu vyenye
mwanga unaomwezesha dereva na abiria kufurahia mwonekano wa pande zote.
Meneja
mauzo wa Diamond Motors, Reena Ganatra alisema Gari hilo lenye luninga ndogo inayocheza
DVD, iPods, Bluetooth na sauti kutoka vyanzo mbalimbali ni maalumu kwa vijana
wa kisasa na familia kwani Mitsubish ASX
limetengenezwa na teknolojia ya MIVEC yenye kulifanya liwe na nguvu ya
150 ps katika 6,000 rpm na nguvu ya kuzunguka kwa mwendokasi mkubwa na kwamba
limetengenezwa maalum kutumia mafuta kidogo.
“ASX
ni mwanzo tu, tunazo aina nyingine za magari kama kama Pajero ambayo
tunakaribia kuyatambulisha sokoni ili kuwapatia watanzania magari imara na
yenye kuaminika kutoka Mitsubishi” Alisema Ganatra.
ASX
toleo la 2015 limebuniwa kwa ubora wa hali ya juu na imara likiwa na bodi gumu
pia lina mfumo maalumu usiotegemea funguo hivyo kumfanya mwendeshaji kuwasha
injini kwa kubofya kitufe.
“ASX kutoka Mitsubishi, imetengenezwa maalumu
kukidhi mazingira ya Tanzania hasa mijini kama Dar es Salaam ambapo muda wowote
dereva wa kawaida anatoka kwenye barabara nzuri na kuingia kwenye barabara
zenye makorongo” alisema Ganatra
Injini
ya gari hilo ambayo ni 2.0-liter imeunganishwa INVECS-III CVT inayoisaidia
mwendelezo wake katika kubadili mwendo pamoja na uimara wa usukani unaosaidia
mikono ya dereva kuwa salama hata
anapokuwa katika mwendo mkali.
Hansa
Group inayofanya biashara kama Diamond Motors Limited, imekuwa ikifanya kazi ya
katika sekta ya usafirishaji tangu mwaka 1980, ikitoa huduma kwa wasambazaji na
wadau wa usafiri.Kampuni hiyo huhusika na bidhaa/ huduma mbalimabali. Shughuli
za Hansa Group zimesambaa karibu nchi zote za jumuia ya Africa ikitoa huduma
kama vile za uchimbaji, Umeme, Mafuta na Gesi, Reli,Ulinzi, Ujenzi, Usafiri,
kimataifa na jumuhia za kimataifa.
Diamond Motors wazindua gari jipya la Mitsubishi 2015 ASX jijini Dar es Salaam
Reviewed by crispaseve
on
09:43
Rating:
Post a Comment