MO DEWJI FOUNDATION YAMPATIA BAISKELI KIJANA ALIYEPOOZA MGUU
Mtendaji
Mkuu wa MO DEWJI FOUNDATION, Gerald Mgesi David akimkabidhi rasmi
kijana Paulo Ezekiel (23) msaada wa baiskeli ya magurudumu matatu
(tricycle) itakayomsaidia katika kutembelea kwenye shughuli zake za kila
siku.
Na Andrew Chale wa Modewji blog
Taasisi
ya MO DEWJI FOUNDATION inayojishughulisha na miradi ya kusaidia jamii
Tanzania katika masuala mbalimbali ikiwemo Afya, elimu na maji mwishoni
mwa wiki imeweza kumpatia kijana Paulo Ezekiel (23) msaada wa baiskeli
ya magurudumu matatu (tricycle) itakayomsaidia katika kutembelea kwenye
shughuli zake za kila siku.
Tukio
hilo la makabidhiano limefanyika katika ofisi za Mo Dewji Foundation
jijini Dar es Salaam ambapo Mtendaji Mkuu wa MO DEWJI FOUNDATION,
Gerald Mgesi David alikabidhi msaada huo kwa kijana Paulo Ezekieli
Akizungumza na Modewjiblog,
Mtendaji mkuu wa Mo Dewji Foundation amesema, waliguswa na usumbufu
aliokuwa anaupata kijana na hivyo kuona ni vyema kumsaidia ili aweze
kumudu kuendesha shughuli zake za kila siku. Mo Dewji
Foundation imejikita katika kutekeleza miradi ya kijamii ambayo inalenga
kusaidia jamii ya kitanzania katika kujikwamua katika hali ya umaskini
na kuinua kipato.
Kijana Paulo Ezekiel (kulia) akiwa kwenye mahojiano na mwandishi wa habari wa modewjiblog, Andrew Chale.
Kijana Paulo Ezekiel:
Kwa
upande wake, kijana Paulo Ezekiel ambaye muda mfupi baada ya
kukabidhiwa baiskeli hiyo, alifanya mahojiano maalum na mtandao huu
ambapo alieza kuwa, tatizohilo la kulemaa mguu, lilimtokea ghafla wakati
yupo mitaa ya Kariakoo kwenye shughuli zake binafsi.
“Nakumbuka
nilikuwa kwenye matembezi maeneo ya Kariakoo, ghafla nilipata kuhisi
hali ya kupooza mguu mmoja wa kulia na kupoteza nguvu wasamaria wema
waliniokota na kunipeleka Muhimbili” anaeleza Paulo Ezekiel.
MO DEWJI FOUNDATION YAMPATIA BAISKELI KIJANA ALIYEPOOZA MGUU
Reviewed by crispaseve
on
02:10
Rating:
Post a Comment