Header AD

KATIBU MKUU WA CCM,NDUGU KINANA AMALIZA ZIARA YAK YA SIKU 9 MKOANI DODOMA,KESHO KUUNGURUMA JIJINI ARUSHA


 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia katika mkutano wa hadhara jioni ya leo katika uwanja wa sabasaba, wilayani Kondoa, wakati wa ziara ya siku tisa iliyomalizika leo mkoani Dodoma ya kuimarisha uhai wa chama, kukagua miradi inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya Uchaguzi ya CCM, pamoja na kusikiliza kero za Wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.

Katika ziara yake hiyo aliyoambatana na Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye ilikuwa ya mafanikio makubwa, kwani msafara wake umetembelelea Wilaya 7 na majimbo 9 ya uchaguzi kwa kuzunguka jumla ya Km, 2289.

Akizungumza katika mkutano wa kuhitimisha ziara hiyo mjini Kondoa, Nape alisema kuwa katika mkoa huo tayari wamefanya mikutano 91, ambapo 82 ya hadhara na 9 ya ndani. Pia wamekagua jumla ya miradi 73 ikiwemo 62 ya maendeleo na 11 ya chama,Nape akaongeza kuwa katika ziara hiyo imefanikiwa kuongeza wanachama wapya wapatao 8245

Kesho Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana na Nape Nnauye wanaanza ziara ya kikazi katika Mkoa wa Arusha, ambapo wataanzia Jimbo la Monduli linaloongozwa na Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa ambaye ni mbunge wa jimbo hilo.
 Mbunge wa Jimbo la Kondoa, Zabein Mhita akijiandaa kupiga magoti  ikiwa ni ishara ya kumuomba Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana kusaidia kutatua tatizo la maji katika Mji wa Kondoa
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi,Nape Nauye akihutubia katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa sabasaba,jioni ya leo wilayani Kondoa.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akihutubia katika mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Kinyasi, Kata ya Kwadelo, ambapo amemshauri Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro
 Nyalandu na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi pamoja na wakuu wa mikoa minne ya Dodoma, Manyara, Morogoro na Tanga kukka pamoja kupata suluhisho la migogoro inayoendelea ya Wakulima na Wafugaji pamoja na askari wa Wanyamapori kuwashambulia wananchi na hata kufikia kuwaua kwa risasi ambazo maganda yake walimuonesha Komredi Kinana katika mkutano huo. 
Ndugu Kinana akihutubia katika Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Kondoa.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akivalishwa mgolole ikiwa ni heshima kubwa ya wazee wa kijiji cha Changaa,wilaya ya Kondoa
Mkuu mpya wa Wilaya ya Kondoa, Shaban Kisu akijitambulisha
  Nyalandu na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi pamoja na wakuu wa mikoa minne ya Dodoma, Manyara, Morogoro na Tanga kukka pamoja kupata suluhisho la migogoro inayoendelea ya Wakulima na Wafugaji pamoja na askari wa Wanyamapori kuwashambulia wananchi na hata kufikia kuwaua kwa risasi ambazo maganda yake walimuonesha Komredi Kinana katika mkutano huo. 
Ndugu Kinana akihutubia katika Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Kondoa.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akivalishwa mgolole ikiwa ni heshima kubwa ya wazee wa kijiji cha Changaa,wilaya ya Kondoa
Mkuu mpya wa Wilaya ya Kondoa, Shaban Kisu akijitambulisha
wakati wa mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Changaa, Kondoa leo. Kisu ambaye alikuwa mtangazaji wa TBC ameteuliwa hivi karibuni na Rais kushika wadhifa huo.
Mkuu mpya wa Mkoa wa Dodoma Mh.Chiku Galawa akijitambulisha wakati wa mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Changaa, Kondoa leo. Mh.Galawa alikuwa mkuu wa mkoa wa Tanga.
 Mbunge wa Jimbo la Kondoa Zabein Mhita akielezea utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi wakati wa mkutano uliofanyika katika Kijiji cha
 Changaa.
Baadhi ya Wananchi wa Kijiji cha Kinyasi, Kata ya Kwadelo, wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alipowahutubia,Kinana amemshauri Waziri wa Maliasili na
 Utalii, Lazaro Nyalandu na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi pamoja na wakuu wa mikoa minne ya Dodoma, Manyara, Morogoro na Tanga kukaa pamoja kupata suluhisho la migogoro inayoendelea ya Wakulima na Wafugaji pamoja na askari wa Wanyamapori kuwashambulia wananchi na hata kufikia kuwaua kwa risasi ambazo maganda yake walimuonesha Komredi Kinana katika mkutano huo.
Baadhi ya Wananchi wa Kijiji cha Kinyasi, Kata ya Kwadelo, wakimsikiliza Katibu
 Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alipowahutubia,
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akionyesha maganda ya risasi yaliyotumiwa na askari Nyama Pori na kuwajeruhi wananchi
Baadhi ya Wananchi wa Kijiji cha Kinyasi, Kata ya Kwadelo, wakimsikiliza Katibu
 Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alipowahutubia,
Wananchi wa Kata ya Kwadelo wakinyoonsha mikono juu kukikubali Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuliko vyama vingine vya siasa.
Baadhi ya Wazee wa kijiji cha Kwadero wakimsikiliza Katibu Mkuu wa
CCM Ndugu Kinana alipokuwa akiwahutubia jioni ya leo.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana haonekani pichani akishiri kuweka jiwe la msingi kwa ofisi ya CCM wilayani Kondoa.
Moja ya Jengo la Kituo cha Kilimo ambalo Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana pia alikagua.
KATIBU MKUU WA CCM,NDUGU KINANA AMALIZA ZIARA YAK YA SIKU 9 MKOANI DODOMA,KESHO KUUNGURUMA JIJINI ARUSHA KATIBU MKUU WA CCM,NDUGU KINANA AMALIZA ZIARA YAK YA SIKU 9 MKOANI DODOMA,KESHO KUUNGURUMA JIJINI ARUSHA Reviewed by crispaseve on 09:47 Rating: 5

No comments

Post AD