TANZANIA, JAPAN WATILIANA SAINI UJENZI WA KITUO CHA UFUNDI STADI ILEJE
Signing the grant contract, witnessed by Hon. Janet Mbene, Deputy
Minister of Industry and Trade, and Hon. Rosemary Senyamule, Ileje
District Commissioner. Front line from the left: Mr. Mussa Otieno,
District Executive Director, Mr. Simon Mwango'nda, Executire Director of
the recipient organisation, Integrated Rural Development Organisation,
Mr. Kazuyoshi Matsunaga, Chargé d'affaires of the Embassy of Japan.
MKATABA
wa Ujenzi wa kituo cha mafunzo ya ufundi stadi katika Wilayani Ileje,
Mkoani Mbeya umetiwa saini. Mradi huo uliobuniwa na Naibu waziri wa
Viwanda na Biashara, Janet Mbene na Simon Kamiyoge umelenga kuwawezesha
wakazi wa Ileje kuwa na taaluma ya ufundi na baadae kutumika kuendelea
wilaya hiyo.
Mkataba
huo ulitiwa saini kati ya Kazuyoshi Matsunaga wa ubalozi wa Japan
nchini na na Mwakilishi wa Integrated Rural Development Organisation
(IRDO) Simon Kamiyoge wakishuhudiwa na Naibu waziri wa Viwanda na
Biashara, Mh. Janet Mbene , Mbunge wa Ileje Rosemary Staki na Mkuu wa
wilaya ya hiyo Mohamed Maliyao Mwala, na Mwenyekiti wa halmashauri ya
Ileje Musa J. Otieno na maofisa wengine wa wilaya hiyo.
Kaimu
Balozi wa Japan Kaziyoshi alisema amefurahishwa sana kutiwa saini kwa
mkataba huo kwa kuwa unamkumbusha miaka 70 iliyopita katikati ya vita
kuu ya pili ya dunia ambapo Japan ilijikuta katika uharibifu mkubwa
pamoja na kubomolewa kwa majengo ya shule.
Alisema
katika vita hiyo Japan ilijikuta si tu hawana shule bali hakukuwa na
nyumba, maji, umeme hamna chochote kile lakini sasa hivi Japan ni ya
tatu kiuchumi.
Discussion between Mr. Kazuyoshi Matsunaga, Chargé d'affaires of the
Embassy of Japan, and Hon. Janet Mbene, Deputy Minister of Industry and
Trade. From left: Hon. Janet Mbene, Deputy Minister of Industry and
Trade, Hon. Rosemary Senyamule, Ileje District Commissioner, Hon.
Mohamed Maliyao Mwala, Chairperson of Ileje District Council, Mr. Mussa
Otieno, District Executive Director, Mr. Kazuyoshi Matsunaga, Chargé
d'affaires of the Embassy of Japan.
TANZANIA, JAPAN WATILIANA SAINI UJENZI WA KITUO CHA UFUNDI STADI ILEJE
Reviewed by crispaseve
on
04:02
Rating:
Post a Comment