WAFANYABIASHARA MANISPAA YA SUMBAWANGA WALALAMIKIA KODI MBALIMBALI SERIKALINI, MKUU WA MKOA WA RUKWA ENG. STELLA MANYANYA AWATAKA KUWA WAZALENDO KULIPA KODI KWA HIARI KUJENGA NCHI YAO
Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya akisikiliza risala ya umoja wa
wafanyabiashara wa Manispaa ya Sumbawanga iliyokuwa ikisomwa kwake na
Mwenyekiti wa umoja huo Ndugu Willington Kiziba Ndyetabura (Kulia).
Katika risala hiyo yalikuwepo malalamiko mbalimbali ikiwemo ya matumizi
ya mashine za EFD ambapo ni pamoja na gharama kubwa za mataengenezo, Ada
ya ukaguzi wa majanga ya moto(Fire), Kupanda mara mbili kwa
kodi ya mapato kwa wafanyabiashara wadogo na Ulinzi na Usalama kwa
wafanyabiashara. Wafanyabiashara hao walihoji n ivigezo gani
vilivyotumika kupandishwa kwa kodi hiyo.
Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya akizungumza na umoja wa
wafanyabiashara wa Manispaa ya Sumbawanga tarehe 19/03/2015 katika
mkutano wa pamoja wa kusikiliza kero zao mbalimbali uliofanyika katika
ukumbi wa Upendo View katikati ya Mji wa Sumbawanga. Wafanyabiashara hao
waliomba kuonana na Mkuu huyo wa Mkoa ambapo pamoja na mambo mengine
aliwataka wafanyabiashara hao kuwa wazalendo kwa kulipa kodi kwa hiari
ili kuchangia maendeleo ya Mkoa na taifa kwa ujumla.
Katika
kujibu kero zao mbalimbali alisema kuwa, zile kero ambazo haziwezi
kutatuliwa mpaka yafanyike mabadiliko ya sheria atayachukua na
kuyafikisha sehemu husika na pindi marekebisho yatakapohitajika
yatafanyiwa kazi, aliwataka pia wafanyabishara hao watii sheria
mbalimbali za kodi ikiwemo kuchangia ada ya ukaguzi wa majanga ya moto
ili kuimarisha jeshi la zimamoto ambalo linahitaji maboresho makubwa kwa
usalama wa wananchi na malizao.
Kuhusu
hali ya ulinzi na usalama katika Mkoa wa Rukwa alisema kwa sasa hali ni
shwari ukilinganisha na kipindi cha nyuma ambapo hivi karibuni wahalifu
mbalimbali waliokuwa wakisumbua wamekamatwa. Aliwataka wafanyabiashara
hao kuwa walinzi namba moja wa amani katika Mkoa wa Rukwa kwa kutoa
taarifa zozote zenye dalili za uhalifu au za watu wanaowatilia mashaka.
Sehemu ya wafanyabiashara wa Mjini Sumbawanga wakifuatilia moja ya mada katika Mkutano huo.
Mhe. Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania kutoka Naibu Kamishna wa Polisi kuwa Kamishna wa
Polisi. Hafla hiyo fupi ilifanyinyika jana Makao Makuu ya Polisi jijini
Dar es Salaam.(Picha na Frank Geofray-Jeshi la Polisi).
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi
ya Ulinzi na Usalama mhe. Dkt Jakaya Mrisho Kikwete, amewapandisha vyeo
maafisa watatu (3) wa Jeshi la Polisi kutoka cheo cha Naibu Kamishina wa
Polisi (DCP) kuwa Kamishina wa Polisi (CP) na maafisa wengine 14 kutoka
cheo cha Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) kuwa Naibu
Kamishina wa Polisi (DCP).
Maofisa waliopandishwa vyeo kutoka cheo cha Naibu Kamishina wa Polisi
(DCP) kuwa Kamishina wa Polisi (CP) ni pamoja na Kenneth Kasseke, Elice
Mapunda na Diwani Athumani.
Maofisa wengine waliopandishwa cheo kutoka Kamishina Msaidizi Mwandamizi
wa Polisi (SACP) kuwa Naibu Kamishina wa Polisi (DCP) ni pamoja na
Godluck Mongi, Ally Lugendo, Salum Msangi, Faustine Shilogile, Maulid
Mabakila, Albert Nyamhanga, Daniel Nyambabe, Salehe Ambika, Robert Boaz
na Gabriel Semiono. Pia wamo kamanda wa Polisi mkoa wa Simiyu Charles
Mkumbo, kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza Valentino Mlowola, kamanda wa
Polisi mkoa wa Arusha Liberatus Sabas na kamanda wa Polisi mkoa wa Ilala
Maria Nzuki.
Aidha, mhe. Rais amempandisha Juma Yusuf Msige kutoka cheo cha kamishina
msaidizi wa Polisi (ACP) kuwa kamishina msaidizi mwandamizi wa Polisi
(SACP).
Kufuatia kupandishwa vyeo kwa maafisa hao wa Jeshi la Polisi, Mkuu wa
Jeshi la Polisi nchini IGP Ernest Mangu katika hafla fupi ya kuwaapisha
makamishina hao wapya, amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Mhe. Dkt
Jakaya Mrisho Kikwete kwa kutambua mchango wa Jeshi la Polisi katika
kuimarisha ulinzi na usalama wa raia na mali zao.
Aidha, IGP Mangu amewapongeza maofisa wote waliopandishwa vyeo na
kuwataka kuendelea kufanya kazi kwa bidii na weledi mkubwa ili kuwa
chachu ya mabadiliko katika kuimarisha usalama wa raia na mali zao. IGP
Mangu aliongeza kuwa, cheo ni dhamana na kuwataka kuwa mfano mzuri
katika utekelezaji wa majukumu yao na usimamizi kwa walio chini yao.
Imetolewa na:
Advera Bulimba -SSP
Msemaji wa Jeshi la Polisi.
Copy and WIN : http://ow.ly/KfYkt
Copy and WIN : http://ow.ly/KfYkt
WAFANYABIASHARA MANISPAA YA SUMBAWANGA WALALAMIKIA KODI MBALIMBALI SERIKALINI, MKUU WA MKOA WA RUKWA ENG. STELLA MANYANYA AWATAKA KUWA WAZALENDO KULIPA KODI KWA HIARI KUJENGA NCHI YAO
Reviewed by crispaseve
on
07:54
Rating:
Post a Comment