viongozi wa dini wasiwapotoshe wananchi kuhusiana na kuwapo kwa masuala ya dini katika katiba -Mangula
Makamu
mwenyekiti wa CCM bara Philip Mangulla akizungumza na wanafunzi na
waalimu shule ya Hagafilo mkoani njombe kuhusian ana katiba pendekeza na
utofauti kati ya katiba pendekezwa na ya sasa.
wanafunzi
na waalimu wakimsikiliza Makamu mwenyekiti wa CCM bara Philip Mangula
juzi wakati akiwapa ufafanuzi wa katiba Pendekezwa.(picha na furaha
eliabu wa www.eliabu.blogspot.com)
Na
Furaha Eliab, Njombe
MAKAMU
mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Bara, Philip Mangula amesema kuwa
viongozi wa dini wasiwapotoshe wananchi kuhusiana na kuwapo kwa masuala ya dini
katika katiba pendekezwa na kuwataka wamuonyeshe kipengele kinacho taja masuala
ya dini na mahakama ya Kadhi.
Akizunzungumza
na wanafunzi wa sekondari, Chuo na walimu katika shule ya Hagafilo Mkoani
Njombe wakati akitoe elimu ya katiba pendekezwa , amesema kuwa ameisoma katika
yote na hajaona kipengele kinacho zungumzia masuala ya udini wala mahakama ya
kadhi.
Lakini
hata hivyo viongozi wa dini wanapinga mswada wa mahakama ya kadhi kupitishwa
bungeni na kuwa sheria.
Amesema
kuwa alikuwa katika kanisa moja anako Sali mchungaji wake alisema kuwa waumini
wasiipegie kura katiba pendekezwa kwa kuwa ina masuala ya Mahakama ya Kadhi
alipo muuliza ni katika kipengele gani kinacho zungumzia mahakama hiyo
mchungaji huyo hata kipengele hicho alisema hakifahamu.
Amesema
kuwa katiba hiyo haina kipengele hata kimoja kinachozungumzia dini yoyote na
kunakipengele kinacho zungumzia utawala wa sheria na kuwapo kwa mahakama huru
Amesema
kuwa katika katiba pendekezwa kuna misingi ya utawala bora na umiliki wa arhi
na kuwa ardhi hiyo inatunza na kuwa ni mali ya mtanzania wa kizazi cha sasa na
cha baadae.
Katika hatua
nyingine Mangula ameungana na kauli ya kiongozi katoriki Kadrinari Polinal
Pengo kuhusiana na kuwahusu wananchi kuchukua maamuzi yao wenyewe juu ya kupiga
kura ya ndio au hapana.
viongozi wa dini wasiwapotoshe wananchi kuhusiana na kuwapo kwa masuala ya dini katika katiba -Mangula
Reviewed by crispaseve
on
10:14
Rating:
Post a Comment