WENGI WANUFAIKA NA SEMINA YA KILIMO NA UFUGAJI WA KISASA ILIYO ENDESHWA NA MJASIRIAMALI BI. MARY DAVID JIJINI DAR
Baadhi ya wanasemina wakiwa katika Picha ya pamoja
Kilimo
na Ufugaji wa Kisasa kwa maendeleo ya Jamii na kukataa umasikini kwa
kujiajili ndiyo kauli kuu iliyotawala katika Semina ya Kilimo na Ufugaji
wa kisasa iliyofanyika Jijini Dar es salaam ambapo washiriki walipata
mafunzo na Elimu Bora juu ya Kilimo bora cha kisasa pamoja na ufugaji
Semina iliyo ongozwa na Mjasiriamali mwanamke ambaye amethubutu Bi. Mary
David Kinong'o.
Katika
Semina hiyo kulikuwa na mafunzo mbalimbali ikiwa ni pamoja na Kilimo
cha kisasa cha kutumia Green houses ambapo , wanasemina walipata elimu
ya umuhimu wa kilimo hicho ambacho hakichukui nafasi kubwa na kinaweza
kufanyika mahali popote na kwa gharama nafuu ambapo kilimo kama cha
Nyanya, Matunda na Mboga mboga kinaweza kikafanyika katika Green Houses.
Pia
walipata elimu juu ya ufugaji wa Samaki, Kuku, Kware pamoja na Matumizi
ya Mashine za Kisasa za Kutotolea mayai Incubator, Chicken Cages za
kisasa ambazo zinasaidia kuwatunza kuku vizuri na kupata faida zaidi,
Mashine za kunyonyolea kuku na kutengenezea chakula cha kuku ili mfugaji
asipate shida wakati wa kutafuta wapi apate mahali pa kufanya hayo na
badala yake kuwa nayo mwenyewe nyumbani.
Mwisho
Mwendesha semina Bi. Mary David Aliwasisitiza watanzania kuwa wanaweza
kuwa wajasiliamali na kujitegemea pia kupata kipato kikubwa kama
wakifuata hatua bora za kilimo na ufugaji wa kisasa.
Tembelea Libeneke lake la: www.kukuprojecttz.blogspot.com
WENGI WANUFAIKA NA SEMINA YA KILIMO NA UFUGAJI WA KISASA ILIYO ENDESHWA NA MJASIRIAMALI BI. MARY DAVID JIJINI DAR
Reviewed by crispaseve
on
06:27
Rating:
Post a Comment