NAIBU WAZIRI WA MAJI ATEMBELEA MRADI WA MAJI ZIWA VICTORIA, KAHAMA,SHINYANGA NA KISHAPU
ZIARA
ya naibu waziri ilianzia kwenye chanzo ca maji kitongoji cha Ihelele,
kijiji cha Nyanghomango kwa kugagua chanzo, sehemu ya kutibu maji na
kusukuma maji kisha kuongea na wananchi wa kijiji cha Nysnghomango
Aidha alikagua mradi unaoendelea kujengwa wa kupeleka maji miji ya mwadui, Maganzo na Kishapu.
Mradi huu
mkubwa wa maji unagharimu shilingi bilioni 254 na una uwezo wa kuzalisha
maji lita milioni 120 kwa siku lakini mpaka sasa unazalisha maji lita
milioni 80 tu kwa siku na unahudumia miji ya kahama, shinyanga, Ngudu
,vijiji 55 vilivyopitiwa na bomba.
Kwa mujibu
wa kaimu mkurugenzi wa Kashwasa ambao ndiyo waendeshaji wa mradi huu
injinia Laurance Wasala amesema Mradi huu ni mkubwa na maji yanatosha
kufikisha maji Tabora na miji ya mwadui, mwadui, kagongwa, isaka, Tinde,
Nzega na Igunga.
Akiwa
kijiji cha Nyanghomango naibu waziri wa maji amewahakikishia wananchi
kuwa wizara ya maji inafanya kila linalowezekana likamilishe mradi wa
maji katika kijiji hicho ambacho ndiyo chanzo.
Kuhusu
mradi wa maji kupeleka maji Kishapu, Mwadui na maganzo ameridhishwa na
kazi nzuri inayofanywa na Kashwasa na amehaidi wizara ya maji
itafuatilia fedha wizara ya fedha zilizopitishwa katika bajeti zitumwe
Kashwasa kwa ajili ya ujenzi wa mradi huo.
Naibu waziri wa maji, Amos Makalla akiwa katika chanzo cha maji Ihelele wilaya ya Misungwi.
Naibu waziri wa maji, Amos Makalla akikagua
sehemu ya kutibu na kusukuma maji ihelele kulia kwake ( mwenye shati
jeupe) ni kaimu mkurugenzi wa Kashwasa injinia Laurance Wasala.
Naibu waziri wa maji, Amos Makalla Akihutubia wananchi kijiji cha Nyanghomango.
Naibu waziri wa maji, Amos Makalla akikagua mradi mradi wa Kupeleka maji Mwadui, maganzo na kishapu. Kulia ni mkuu wa wilaya ya Kishapu wilson Nkambaku.
Naibu waziri wa maji, Amos Makalla akionngea na waandishi wa habari kwenye mradi wa maji Kishapu.
Naibu
waziri wa maji Amos Makalla ametembelea mradi mkubwa wa maji toka ziwa
victoria na kuyapeleka miji ya Kahama, shinyanga, Ngudu, Kishapu, vijiji
55 na Tabora.
NAIBU WAZIRI WA MAJI ATEMBELEA MRADI WA MAJI ZIWA VICTORIA, KAHAMA,SHINYANGA NA KISHAPU
Reviewed by crispaseve
on
04:37
Rating:
Post a Comment