SERIKALI KUCHUNGUZA MKATABA WA JENGO LA MACHINGA COMPLEX
Mkuu wa
Mkoa wa Dar es Salaa, Paul Makonda (kulia), akikagua vizimba katika
Jengo la Machinga Complex Dar es Salaam jana, baada ya kufanyika kikao
cha kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa kilichoketi jana kujadili
uendeshaji wa biashara wa katika jengo hilo pamoja na kamati ya mkoa
iliyoundwa kuchunguza mkataba wa jengo.
Mkuu wa
Mkoa wa Dar es Salaa, Paul Makonda akizungumza na wafanyabiashara katika
Jengo la Machinga Complex Dar es Salaam jana, kuhusu uendeshaji wa
jengo hilo.
Makonda
akiwasili katika viwanja vya Jengo la Machinga Complex kuzungumza na
wafanyabiashara na wadau wengine. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala,
Raymond Mushi wengine ni viongozi wa jengo hilo.
Makonda akiangalia Uwanja wa Karume akiwa jengo la Machinga Complex.
Kamanda
wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, CP Simon Sirro akimuaga Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda baada ya kumaliza kuzungumza na
wananchi.
Na Dotto Mwaibale
MKUU wa
Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ameagiza kufanyika kwa uchunguzi
katika ujenzi wa jengo la Machinga Ciomplex ili kubaini uhalali wa
mkataba uliotumika kujenga jengo hilo.Aidha, amebainisha kuwa jengo la
Machinga Complex kwa sasa linadaiwa zaidi ya Sh bilioni 36 kiasi ambacho
ni mara tatu ya thamani halisi ya jengo hilo ambayo ni Sh 12 ambazo
zinatakiwa kulipwa na wafanyabiashara wa jengo hilo.
Makonda
aliyasema hayo Dar es Salaam jana wakati alipotembelea jengo hilo
lililopo Manispaa ya Ilala ili kujionea mazingira ya kufanyia biashara.
Alisema kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa itaanza kufanya uchambuzi wa
mikataba ili kupata uhalali wa gharama na kujua kiwango kinachostahili
kulipwa na wafanyabiashara hao.
Alisema
kamati hiyo ya ulinzi na usalama imekubali kutengeza kamati ndogo
itakayoanza kazi leo ya kuchambua na kuanza mikataba.“Ingekuwa vyema
tungekuwa na mkutano wa kuwasikilizeni na kujua kero zenu, lakini tunayo
sababu moja ya msingi ya kutowasikiliza , kwanza tunatafuta uhalali na
utaratibu wa jengo hili lilivyojengwa.
Katika
maelezo ya awali tuliyoyapata jengo hili uko mkanganyiko mkubwa,
inawezekana ni miongoni mwa mradi mkubwa uliofanyiwa ufisadi Tanzania,
sasa hatuwezi kukaa kusikiliza habari ya kizimba change, kwanza tupate
uhalali wa mkataba uliopelekea kujenga jengo hili,” alisema Makonda.
Alisema
kamati ya wafanyabiashara wa soko hilo itakayoundwa chini ya usimamizi
wake itaanza kazi ya kuchunguza ili kubaini uhalali wa mkataba na kujua
kama waliongia mikataba hiyo walikuwa sahihi.Makonda alitoa rai kwa
wafanyabiashara kuwa rai ya Rais Magufuli ni kuwapigania wanyonge na
kuhakikish awanatoka sehemu moja kwenda nyingine, hivyo wasaidiza wake
kwa kupenda au kutokupenda wana jukumu la kuhakikisha wanafanikisha
hilo.
Hivi
karibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI, George Simbachawene
aliifuta bodi inayosimamia jengo hilo na kumsimamisha kazi meneja
anayesimamia jengo hilo na kumtaka kwenda katika ofisi za jiji kwa ajili
ya kumpangia kazi nyingine.
Katika
hatua nyingine, Simbachawene alilikabidhi jengo hilo kwa Mkuu wa Mkoa wa
Dar es Salaam kwa ajili ya kuandaa mpango wa kuwaingiza wafanyabiashara
bila masharti huku ukiangaliwa utaratibu mpya kwa wafanyabiashara
hao.Katika mkutano wake na Jumuiya ya Wafanyabiashara nchini,
Simbachawene alisema, jengo hilo limekuwa likitumiwa kinyume na lengo
ambalo walitakiwa wafanyabiashara kulitumia kwa gharama kidogo lakini
limekuwa likitumiwa na watu wengine tofauti na wafanyabiashara jambo
ambalo limesababisha kushindwa kulipa deni linalodaiwa na Mfuko wa
Hifadhi ya Jamii (NSSF).
SERIKALI KUCHUNGUZA MKATABA WA JENGO LA MACHINGA COMPLEX
Reviewed by crispaseve
on
07:11
Rating:
Post a Comment