WABUNGE WA EALA-TANZANIA WATEMBEELA CLOUDS MEDIA GROUP NA KUPEWA UJUMBE MZITO
Wabunge
wa bunge la Afrika Mashariki kutoka Tanzania, na wafanyakazi wa Clouds
Media Group, akiwemo mchekeshaji maarufu Bishanga Bashaija, wakiwa
kwenye moja ya studio za Clouds Media Group, wakati wa kipindi maarufu
cha Leo Tena, Aprili 22, 2016.
NA
K-VIS MEDIA/Khalfan Said
WABUNGE
wa bunge la Afrika Mashariki (EALA), kutoka Tanzania, wametembelea Clouds Media
Group,Mikocheni jijini Dar es Salaam
Aprili 22, 2016 ikiwa ni sehemu
ya ziara yao ya takriban siku 20 kutembelea vyombo vya habari kwa nia ya
kuvishirikisha vyombo hivyo kutoa elimu kwa wananchi kuchangamkia fursa
zilizopo kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group, inayomiliki kituo cha radio, Clouds FM, Clouds
TV, Bw. Ruge Mutahaba, amewaeleza wabunge hao walioongozwa na mwenyekiti wao
Mh. Chrles Makongoro Nyerere kuwa, Tanzania inakabiliwa na tatizo kubwa la
kutogeuza vipaji kuwa biashara na hivyo kujiingizia kipato.
Ruge
amewahimiza wabunge hao kushawishi serikali ya Tanzania kurekebisha sera zake
za kuwawezesha wananchi na kuwajengea uwezo wa kuvitumia vipaji walivyojaaliwa
na Mwenyezimungu ili kujiingizia kipato.
Akielezea
nia ya ziara hiyo, Mwenyekii Mh. Makongoro Nyerere alisema, wabunge kutoka nchi
wanachama walipewa jukumu la kuwatembelea wananchi wa nchi watokako ili kwahimiza
kuchangamkia fursa zilizopo kwenye Jumuiya hiyo ambayo kwa sasa ina jumla ya
wanachama sita, Tanzania, Kenya Uganda, Rwanda, Burundi na Sudani Kusini.
“Jumuiya
ya Afrika Mashariki ina soko la kutosha na wananchi wa Jumuiya hii wanyo fursa
ya kwenda kufanya shughuli za kiuchumi bila kizuizi chochote ikiwemo biashara
na kufanya kazi hivyo ni wakati wa watanzania kuacha kulalamika na kuchangamkia
fursa hiyo.” Alisema Mh. Makongoro.
Pamoja
na Mh. Makongoro, wabunge wengine ni pamoja na Mh. Shy-Rose Bhanji, na Mh.
Nderaikindo Kessy.
Mkurugenzi
wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group, Bw. Ruge Mutahaba,
(kulia), akitoa maelezo ya uendeshaji wa kampuni hiyo, wakati wabunge wa
bunge la Afrika Mashariki (EALA-Tanzania), walipotembelea studio za
Clouds radio/TV Mikocheni jijini Dar es Salaam Aprili 22, 2016. Kutoka
kushoto ni Mwenyekiti wa wabunge hao Mh. Charles Makongoro Nyerere, Mh.
Nderaikindo Kessy, na Mh. Shy-Rose Bhanji.
Mtangazaji wa kipindi cha Leo Tena, Gea Habib
Mwenyekiti Mh. Charles Makongozo Nyerere (kulia) akizungumza kwenye kipindi cha Leo tena
WABUNGE WA EALA-TANZANIA WATEMBEELA CLOUDS MEDIA GROUP NA KUPEWA UJUMBE MZITO
Reviewed by crispaseve
on
07:02
Rating:
Post a Comment