WAZIRI WA CZECH REPUBLIC NA UJUMBE WA WAFANYABIASHARA WATEMBELEA KIWANDA CHA MAZIWA MILKCOM KIGAMBONI
Marian
Jureck Waziri wa Kilimo wa wa Jamhuri ya watu wa Czech Republic
akiangalia chakula cha Ng'ombe wakati alipotembelea mashamba ya ng'ombe
na kiwanda cha MilkCom kinachomilikiwa na makampuni ya OilCom Group
kilichopo Kigamboni wilayani Temeke jijini Dar es salaam akiongozana na
ujumbe wa wafanyabiashara kutoka nchini humo, Ujumbe huo ulikuja nchini
kwa lengo la kuangalia fursa za uwekezaji zilizopo nchini Tanzania na
ushirikiano wa kibiashara kati ya nchi hizi mbili.(PICHA NA JOHN
BUKUKU-FULLSHANGWE-KIGAMBONI)
Marian
Jureck Waziri wa Kilimo wa wa Jamhuri ya watu wa Czech Republic
akiongozwa na Mkurugenzi wa kiwanda cha Milkcom Bw. Salum Nahdi wakati
alipokuwa akitembelea kiwanda hicho.
Baadhi ya ng'ombe katika shabla la kampuni ya MilkCom
Mkurugenzi
wa Kiwanda cha Milkcom Bw. Salum Nahdi kulia, Mh. Balozi wa Heshima wa
Jamhuri ya Czech Republic nchini Tanzania Mh.John Chaggama na SAid Nahdi
Mkurugenzi wa Makampuni ya OilCom Group wakifurahia jambo wakati wa
ziara hiyo ya ujumbe wa Czech Republic.
Baadhi ya wafanyabiashara hao wakikagua eneo la kukamulia maziwa.
Dk.
Sajeev Kumar Meneja wa Shamba la mifugo akitoa maelezo kwa Marian Jureck
Waziri wa Kilimo wa wa Jamhuri ya watu wa Czech Republic na ujumbe wake
wakati alipotembelea shamba hilo.
Marian
Jureck Waziri wa Kilimo wa wa Jamhuri ya watu wa Czech Republic
akiuliza jambo wakati alipotembelea shamba la ng'ombe la Milkcom.
Meneja
wa Shamba la ng'ombe la Milkcom akitoa maelezo kwa Marian Jureck Waziri
wa Kilimo wa wa Jamhuri ya watu wa Czech Republic na ujumbe wake wakati
alipotembekea katika shamba hilo.
WAZIRI WA CZECH REPUBLIC NA UJUMBE WA WAFANYABIASHARA WATEMBELEA KIWANDA CHA MAZIWA MILKCOM KIGAMBONI
Reviewed by crispaseve
on
04:34
Rating:
Post a Comment