UFUATILIAJI WA AGENDA 2030 UNAHITAJI TAKWIMU SAHIHI-TANZANIA
Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako
Manongi akizungumza wakati wa mkutano wa 49 wa Kamisheni ya Umoja wa
Mataifa Kuhusu Idadi ya watu na Maendeleo. Pamoja na Mambo mengine,
Balozi anayeongoza ujumbe wa Tanzania katika Mkutano huo amesema, ili
ufuatiliaji wa utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu
panahitajika taarifa sahihi za takwimu.
Sehemu ya wajumbe wanaohudhuria Mkutano wa Kimesheni ya Umoja wa Mataifa kuhusu Idadi ya watu na Maendeleo.
Na Mwandishi Maalum,
New York
Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, imesema takwimu sahihi zitahitajika katika kufuatilia
utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu maarufu kama Agenda 2030.
Hayo
yameelezwa siku ya jumatano na Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa,
Balozi Tuvako Manongi, wakati wa
Mkutano wa 49 wa Kamisheni ya
Umoja wa Mataifa kuhusu Idadi ya Watu na
Maendeleo ( CPD), mkutano unaoendelea hapa Umoja wa Mataifa.
Balozi
Manongi anayeongoza ujumbe wa Tanzania katika mkutano huo, amesema,
hapana shaka kwamba ili nchi
iwe na takwimu sahihi,
zenye viwango vinavyokubaliwa kitaifa na kimataifa panahitajika
ushirikiano baina ya Idara za Kitaifa za Takwimu, Serikali na washirika wa maendeleo.
“Upatikanaji
wa takwimu zenye viwango katika utekelezaji wa
malengo ya maendeleo endelevu unatutaka tuwe wabunifu na tuboreshe mifumo yetu ya takwimu. Na katika hili, tusijidanganye, haya yote yanahitaji
uwekezaji wa raslimali fedha na utaalam,
patahitajika ushirikiano ambao utasaidia kuimarisha takwimu na kusaidia
utekelezaji wa Agenda 2030”.
Akaeleza Balozi Manongi.
Vilevile
Mwakilishi huyo wa Tanzania, akaongeza
kuwa takwimu sahihi zina uwezo wa kuleta
tofauti mkubwa kwa vile zinawasaidia watendaji
wa serikali katika upangaji wa sera na zinatoa ushahidi wa wapi
palipofanikiwa na wapi pana matatizo au
mapungufu.Na akasisitiza kwa kusema “
Takwimu sahihi zinasaidia uwazi na kubwa zaidi uwajibikaji”.
Akizungumzia
Zaidi nafasi ya takwimu sahihi na zenye
viwango, Balozi Manongi amesema, Tanzania inapenda kusisitiza tena umuhimu wa
ukusanyaji wa takwimu kuhusu idadi ya
watu kwa kile anachosema ni nguzo
muhimu katika siyo tu ufuatiliaji wa utekelezaji wa
maazimio ya Mkutano wa Kimataifa wa Idadi ya watu na Maendeleo lakini pia utekelezaji wa Ajenda 2030.
Akifafanua
Zaidi kuhusu idadi ya watu, Balozi amesema, Tanzania ni kati ya nchi zenye
ongezeko kubwa la idadi ya watu na hususaji
vijana wanaoingia katika soko la ajira.“Ongezeko
la vijana lina fursa na changamoto pia.
Tunatambua kwamba ili nchi yetu inufaike
na uwepo wa idadi kubwa ya vijana tunahitaji kuwa na mipango na sera madhubuti, ikiwa ni pamoja na kuwapatia
mafunzo na stadi ambazo zitaiwezesha
serikali kuvuna utaalamu na ujuzi wao” akabainisha Balozi.
Pamoja
na ongezeko la idadi kubwa ya vijana,
Balozi Manongi amesema kuna ongezeko
pia la wazee wa miaka 60 na kuendelea hali inayoongeza mahitaji ya huduma za
jamii na hususani afya. “ Ndiyo maana
tunatambua muingiliano wa idadi ya watu na maendeleo”.
Pamoja
na kuzungumzia changamoto mbalimbali za
ukusanyaji wa takwimu sahihi na zenye ubora,
Balozi amewaeleza wajumbe wa mkutano huo kwamba, Serikali ya Tanzania imeendelea na
juhudi za kuiwezesha Idara
ya Taifa ya Takwimu, ikiwa ni pamoja na kuiwezesha kisheria kuwa
chombo pekee chenye mamlaka ya utoaji
na usambazaji wa taarifa zinazohusiana na masuala ya takwimu.
Akatumia
nafasi hiyo kutambua siyo tu mchango wa
serikali Kuu bali pia wadau mbalimbali
wa maendeleo na ambao wamekuwa wakisaidia katika eneo hilo.
Awali
akifungua mkutano huo wa 49 wa Kamisheni
ya Umoja wa Mataifa ya Idadi ya Watu na Maendeleo.Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki
Moon amesema watu wasipohesabiwa
wanatengwa na kwamba watu ni kiungo muhumu katika utekelezaji wa Agenda
2030.
Akaeleza malengo 17 ya maendeleo endelevu yamejikita Zaidi katika
usawa na kuwa takwimu za idadi ya watu,
tathmini yake na uchambuzi wake ni muhimu sana katika kumaliza au kupunguza
tofauti ya kati ya walionacho na wasionacho.Vilevile
amesema takwimu sahihi zinasaidia katika kuwasaidia na kuwafikia watu walioko
katika maeneo ambayo yahafikiki na hivyo kuwafikishia maendeleo na maisha yenye
hadhi.
UFUATILIAJI WA AGENDA 2030 UNAHITAJI TAKWIMU SAHIHI-TANZANIA
Reviewed by crispaseve
on
04:35
Rating:
Post a Comment