Rais Magufuli atuma salamu za Rambirambi kifo cha Askofu Mathias Issuja
ASKOFU
AFARIKI: Askofu msaafu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dodoma, Mathias Issuja
amefariki usiku wa kuamkia leo katika Hospitali ya Mt. Gaspar, Itigi,
Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemtumia salamu za rambirambi
Rais wa Baraza la Askofu Tanzania (TEC) Mhashamu Tarcisius Ngalalekumtwa kufuatia
kifo cha Askofu Mstaafu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dodoma, Mhashamu Mathias Issuja
Joseph, aliyefariki dunia usiku wa kuamkia leo tarehe 13 Aprili, 2016 Mkoani
Singida.
Baba Askofu Mstaafu
Mathias Issuja aliyekuwa na umri wa miaka 87, amekutwa na mauti katika
Hospitali ya Rufaa ya Mtakatifu Gaspar iliyopo Itigi, wilaya ya Manyoni Mkoani
Singida alikokuwa akipatiwa matibabu.
Katika salamu hizo
Rais Magufuli amesema Askofu Mstaafu Mathias Issuja alikuwa Mzalendo wa kweli,
kipenzi cha watu, aliyefanya kazi kubwa ya kuwajenga watu kiroho na kimwili, na
kamwe mchango wake katika maendeleo ya Elimu, Afya na malezi ya watoto yatima
hautasahaulika.
"Nimepokea
kwa huzuni kubwa taarifa za kifo cha Baba Askofu Mathias Issuja. Kazi kubwa aliyoifanya
duniani kuwahudumia watu kiroho na kimwili ni vigumu kuipima, nitamkumbuka
daima" Amesema Rais Magufuli.
Dkt. Magufuli
amemuomba Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania Mhashamu Tarcisius Ngalalekumtwa,
kufikisha pole nyingi kwa baraza la Maaskofu, Waumini wa Kanisa Katoliki na
wote walioguswa na msiba huo na amemuomba Mwenyezi Mungu aiweke roho ya
Marehemu mahali pema peponi, Amina.
Gerson
Msigwa
Kaimu
Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es
salaam
Rais Magufuli atuma salamu za Rambirambi kifo cha Askofu Mathias Issuja
Reviewed by crispaseve
on
04:36
Rating:
Post a Comment