ILALA YAVUKA LENGO UKUSANYAJI MADAWATI,YABAINI WANAFUNZI HEWA 599 KATIKA SHULE 6

Mkuu
wa wilaya ya Ilala Mh. Sophia Mjema akifafanua jambo alipokuwa
akizungumza na waandishi wa habari mapema leo ofisini kwake Ilala,jijini
Dar wakati alipotangaza kupatikana kwa wanafunzi hewa 599 katika shule 6
za wilaya hiyo ambapo uchunguzi wa wanafunzi wengine hewa bado
unaendelea.
Mkuu
wa wilaya ya Ilala Mh. Sophia Mjema akisisitiza jambo wakati
alipozungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Ilala wakati
alipotangaza kupatikana kwa wanafunzi hewa 599 katika shule 6 za wilaya
hiyo, Kulia ni Katibu Tawala wa Wilaya hiyo Bw. Edward Mpogolo.
Mkuu
wa wilaya ya Ilala Mh. Sophia Mjema akifafanua jambo wakati akizungumza
na waandishi wa habari ofisini kwake Ilala wakati alipotangaza
kupatikana kwa wanafunzi hewa 599 katika shule 6 za wilaya hiyo.
.............................................................
Mkuu
wa Wilaya ya Ilala Mh. Sophia Mjema ametangaza kupatikana kwa wanafunzi
hewa 599 katika shule 6 za wilaya ya Ilala ambazo hakuzitaja, Mjema
amesema baada ya uchunguzi huo kufanyika,wamebainika wanafunzi idadi
hiyo,ambapo wahusika wote watachukuliwa sheria ikiwamo na hatua za
kinidhamu,kwani hayo ni makosa kama yalivyo makosa mengine
Wilaya ya Ilala ina shule za sekondari za serikali 46 na za sekondari 49 ukiacha shule za taasisi binafsi ,zoezi la ukaguzi bado linaendelea katika shule zote za msingi wilayani humo mpaka Septemba mosi mwaka huu ndiyo litamalizika.
Akizungumzia suala la Madawati mkuu wa wilaya huyo, amewapongeza wadau wote waliochangia madawati mpaka kuhakikisha uhaba wa madawati katika wilaya ya Ilala unakwisha, huku kukiwa na ziada ya madawati 2821
Ameongeza kuwa kazi kubwa inayofuatia kwa sasa ni kuongeza vyumba vya madarasa ambapo kazi hiyo inaendelea vizuri .
Mh. Sophia mjema pia amemshukuru Rais Dk. John Pombe Magufuli kwa kuanzisha mkakati wa wadau kuchangia madawati, jambo ambalo limesaidia tatizo hilo kushughulikiwa kikamilifu na wadau mbalimbali, lakini pia akampongeza Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh. Paul Makonda kwa usimamizi thabiti wa utekelezaji wa mkakati huo. jambo ambalo limesaidia wilaya ya Ilala kumaliza kabisa tatizo la uhaba wa madawati katika shule za zake za msingi

Reviewed by crispaseve
on
08:06
Rating:

Post a Comment