KESI YA TUNDU LISSU YAIHIRISHWA
Hakimu
Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi – Kisutu, Yohanne Yongolo ameihairisha kesi
inayomkabili Mbunge wa Singida Mashariki, Mhe Tundu Lissu hadi Septemba 6 mwaka
huu ili kutoa uamuzi wa maombi yaliyoombwa na upande wa mshtakiwa.
Kesi
hiyo imehairishwa leo Jijini Dar es Salaam na Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo kutokana
na kushindwa kufikia muafaka juu ya hoja iliyotolewa na Wakili wa Utetezi,
Peter Kibatala ya kuiomba Mahakama kuleta barua ya maelezo kutoka kwa Afisa wa
Makosa ya Jinai wa Kanda ya Dar es Salaam (ZCO) kabla ya mashahidi wawili
kutoka upande wa Jamuhuri kuongea.
“Naihairisha
kesi hii hadi Septemba 6 ambapo tutatoa uamuzi kulingana na sheria kama Afisa
wa Makosa ya Jinai wa Kanda (ZCO) anatakiwa kuja kutoa ushahidi au kama
mashahidi hawa walioletwa na upande wa Jamuhuri wanajitosheleza”, alisema Yongolo.
Kwa
upande wake Wakili wa Utetezi, Peter Kibatala amesema kuwa maelezo kutoka kwa Afisa
wa Makosa ya Jinai wa Kanda ni ya muhimu kabla ya mashahidi wawili kutoka
upande wa Jamuhuri kuongea pia mshtakiwa hawezi kujitetea bila kupata maelezo
kutoka kwa afisa huyo.
Naye
Wakili wa Serikali Mkuu, Bernad Kongola amesema kuwa Afisa wa Makosa ya Jinai
wa Kanda sio shahidi katika shauri hilo hivyo kisheria hawalazimiki kumleta
afisa huyo kuja kutoa maelezo mbele ya mahakama.
Mnamo Juni 28 mwaka huu, Lissu aliongea maneno ya
kichochezi muda mfupi baada ya kutoka kusikiliza shauri lake katika Mahakama ya
Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam. Maneno hayo yalimsababishia
kufunguliwa kesi ambayo inasikilizwa na Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Yohanne
Yongolo.
KESI YA TUNDU LISSU YAIHIRISHWA
Reviewed by crispaseve
on
06:53
Rating:
Post a Comment