JACQUELINE MENGI AFANYA UZINDUZI WA DUKA LA SAMANI “AMORETTE”
Alhamisi
ya Septemba, 15 inaingia katika historia ya mjasiriamali, Jacqueline
Mengi kwa kufanya uzinduzi wa duka la samani za ndani la Molocaho
Amorette likiwa na vitu ambavyo ni vya pekee kutokana na aina ya
malighafi ambayo wametumia kutengeneza.
Akizungumzia
duka hilo, Bi.Mengi alisema kuwa ilikuwa ni ndoto yake ya muda mrefu ya
kutaka siku moja kuwa na duka kama hilo ambalo litakuwa na samani
ambazo ni ngumu kuzipata sehemu nyingine kutokana na kutengenezwa
tofauti na samani nyingi ambazo zinapatikana madukani.
"Siamini
kama ndoto yangu imetia, kwa kipindi cha miaka iliyopita kuna vitu
nilikuwa nikitamani kuwa navyo nyumbani lakini sikuweza kuvipata
nilipokuwa nikitafuta na hapo ndipo ndoto za kuwa na duka zilipoanzia,
"Nilikuwa
nataka kitu cha tofauti ambacho ni ngumu kukikuta sehemu nyingine
kutokana na kuwa na ubunifu wa kipekee ambao utawavutia wateja wa ndani
ya nchi na nje ya nchi na ninaamini watafurahia," alisema Bi. Mengi.
Aidha
Bi. Mengi alisema kuwa bidhaa ambazo zitakuwa zikipatikana katika duka
la Molocaho - Amorette zimetengenezwa na malighafi kutoka Tanzania kama
mbao za Mninga na hivyo kuwataka Watanzania kuwa wazalendo kwa kutumia
bidaa ambayo imetengenezwa na malighafi za Tanzania.
Mmoja
wa wageni waliohudhuria halfa ya uzinduzi, Faraja Nyalandu alisema kuwa
kwa kijana kama Jacqueline Mengi kuwa na duka kama hilo ni hatua kubwa
ambayo vijana wengi wanatamani kuifikia, kumpongeza kwa juhudi
alizozifanya lakini pia kutoa ushauri kwa wengine ambao wanataka
kufanikiwa.
"Kwanza
nimpongeze Jacqueline amefanya uthubutu na amefanikiwa kuwa na kitu
kama hiki, juhudi yake inaonyesha kuwa kila mtu tu anaweza kufanikiwa
kama akiongeza juhudi katika jambo analotaka kulifanya," alisema Bi.
Nyalandu.
Duka
hilo la kisasa na la aina yake linapatikana Masaki karibu na hoteli ya
Sea Cliff kwenye jengo la "Village Walk" gorofa ya kwanza.
Mrembo
wa taji la Miss Tanzania 2000, Bi. Jacqueline Mengi akizungumza na
wageni walikwa pamoja na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa
uzinduzi wa duka lake la samani za ndani "Amorette" lililopo katika
jengo la Village Walk gorofa ya kwanza karibu na Sea Cliff Hotel, Masaki
jijini Dar es Salaam.
Muonekano wa nje utaokutambulisha hili ndio duka la "Amorette"
Bi. Jacqueline Mengi akikata utepe kuzindua duka lake hilo.
Ha
ha ha ha, sasa mko huru kuingia wageni waalikwa kujionea
yaliyomo,.....Bi. Jacqueline Mengi akifurahi jambo mara baada ya kukata
utepe.
Bi. Jacqueline Mengi akiongozana na baadhi ya wageni waalikwa kuingia ndani ya duka la "Amorette"
Balozi
Juma Mwapachu na baadhi ya wageni waalikwa wakiangalia moja ya meza ya
chakula (dining table) iliyotengenezwa kwa mbao aina ya Mninga baada ya
kuzinduliwa duka hilo lililopo katika jengo la Village Walk, Masaki
jijini Dar.
Wageni waalikwa wakiendelea kukagua samani mbalimbali katika duka hilo.
Bi. Jacqueline Mengi akiwaonyesha mambo mazuri yaliyomo katika duka la Amorette baadhi marafiki waliohudhuria uzinduzi huo.
Bi.
Jacqueline Mengi akizungumza jambo na Balozi Juma Mwapachu wakati
akiwatembeza wageni waalikwa katika maeneo mbalimbali ndani ya duka lake
la Amorette.
Wageni
waalika wakiangalia moja ya kitanda cha aina yake kinachouzwa katika
duka la Amorette lililopo katika jengo la Village Walk, Masaki jijini
Dar es Salaam.
Sehemu maalum ya kitanda hicho ya kuhifadhia mashuka, Blanket pamoja na mito.
Bi. Jacqueline Mengi akipozi katika moja ya samani ndani ya duka lake la Amorette.
Bi. Jacqueline Mengi katika pozi matata ndani ya duka lake la Amorette.
Bi. Jacqueline Mengi akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuzindua duka lake la samani za ndani la Amorette.
Wanahabari na wageni waalikwa wakiwa ndani ya duka la Amorette kujionea bidhaa mbalimbali.
Wageni waalikwa wakiendelea kutazama kitanda hicho cha aina yake.
Sophia Byanaku akijinafasi katika moja ya samani zilizomo kwenye duka la Amorette.
Mmoja wa wageni waalikwa akitazama bidhaa mbalimbali zilizotengenezwa kwa mbao aina ya Mninga ndani ya duka la Amorette.
Baadhi ya samani zilizomo ndani ya duka la Amorette.
Balozi Juma Mwapachu (kushoto) akibadilishana mawazo na mwalikwa mwenzake kwenye uzinduzi wa duka la Amorette.
Mwanadada Monica Joseph akipozi kwenye moja ya bidhaa zilizopo ndani ya duka la Amorette.
Bi. Jacqueline Mengi akipozi kwenye samani moja wapo inayopatikana katika duka lake la Amorette.
Warembo
wakiwa wamepozi kwenye samani zinazopatikana katika duka la Amorette
lililopo ndani ya jengo la Village Walk, Masaki jijini Dar es Salaam.
Wageni waalikwa wakibadilishana mawazo ndani ya duka la Molocaho-Amorette.
Bi. Jacqueline Mengi akiwa kwenye picha ya pamoja na rafiki zake.
Bi. Jacqueline Mengi akibadilishana mawazo na baadhi ya marafiki zake.
Mkurugenzi wa Dorice Mollel Foundation, Dorice Mollel (kulia) katika picha ya pamoja na Mdau Monica Joseph.
Bi. Jacqueline Mengi katika picha ya pamoja na Dorice Mollel.
JACQUELINE MENGI AFANYA UZINDUZI WA DUKA LA SAMANI “AMORETTE”
Reviewed by crispaseve
on
03:07
Rating:

Post a Comment