LHRC WASHEREHEKEA MIAKA 21 NA WATOTO WANAOISHI MAKAO YA TAIFA YA WATOTO WENYE SHIDA KURASINI JIJINI DAR ES SALAAM
Wafanyakazi wa LHRC wakijumuika na
watoto wanaolelewa katika Makao ya taifa ya watoto wenye shida Kurasini
jijini Dar es Salaam jana ikiwa ni sehemu ya kusherehekea miaka 21 tangu
kuanzishwa kwake.
Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC Dk. Helen Kijo-Bisimba (katikati) akiwasaidia watoto kukata keki kusheherekea miaka 21 ya LHRC.
Ofisa
Mfawidhi wa Makao ya Taifa ya Watoto wenye shida Kurasini, Beatrice
Lawrance, akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika Dar es Salaam jana
ikiwa ni sehemu ya maadhimisho hayo.
Na Dotto Mwaibale
KITUO
cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimeiomba serikali kupitia
wizara ya Afya ,Jamii Jinsia ,Wazee na Watoto, pamoja na na Wizara ya
Katiiba na Sheria ,kufanya marekebisho yaSsheria ya Mtoto nakutilia
mkazo malezi bora ya watoto ikiwemo kuweka kipengele kitakacho toa
adhabu kali kwa familia itakayo shindwa kutoa malezibora kwa watoto au
kutelekeza familia.
Akizungumza
katika maadhimisho ya miaka 21 ya kituo cha sheria na haki za
binadamu, yaliyofanyika katika Makao ya Taifa ya Watoto wenye shida
kilichopo Kurasini, Temeke Jijini Dar es salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa
kituo hicho Dk. Helen Kijo-Bisimba alisema kuboreshwa kwa sheria hizo
kutasaidia kupunguza wimbi la watoto wasio na makao maalumu wanao zagaa
kuomba omba mitaani, na ameitaka jamii kushiriki katika kutatua tatizo
la watoto wa mitaani linalozidi kushika hatamu kila siku.
Ofisa
Mfawidhi wa kituo hicho, Beatrice Laurence ame kishukuru kituo cha
sheria na haki za Nina damu kwakuona umuhimu wa kutoka misaada katika
kuwa saidia watoto wanao lelewa hapo nakuwataka watanzania wengine
badala ya kuelekeza nguvu zao pekee kwa wathirika wa tetemeko huko
Kagera kuwa kumbuka na watoto yatima kwani nao wanayo kahitaji ya
kibinadamu.
Kituo
cha Sheria na Haki za Binadamu kilianzishwa Septemba 26, 1995 kwa lengo
la kufanya utetezi kwa watu wenye uhitaji sambamba na kulinda haki za
binadamu nchini.
LHRC WASHEREHEKEA MIAKA 21 NA WATOTO WANAOISHI MAKAO YA TAIFA YA WATOTO WENYE SHIDA KURASINI JIJINI DAR ES SALAAM
Reviewed by crispaseve
on
01:43
Rating:
Post a Comment