SSRA YAWATOA HOFU WANANCHI KUHUSU MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII NCHINI
Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Onorius Njole (kushoto), akitoa ufafanuzi mbalimbali kwenye semina ya siku moja ya wanahabari kuhusu mifuko ya jamii Dar es Salaam leo. Kulia ni Mkuu wa Idara ya Uhusiano na Uhamasishaji, SSRA, Sarah Kibonde.
Mkurugenzi wa Tafiti, Sera na Tathmini wa SSRA, Ansgar Mushi akitoa mada katika warsha hiyo.
Waandishi wa habari wakiwa katika semina hiyo.
Waandishi wakiwa kwenye semina hiyo
Semina ikiendelea.
Waandishi wa habari wakichukua mambo kadhaa kwenye semina hiyo.
Wanahabari wakiwa makini katika semina hiyo.
Maswali yakiulizwa.
Taswira meza kuu katika semina hiyo.
Picha ya pamoja waandishi wa habari na maofisa wa SSRA.
Na Dotto Mwaibale
MAMLAKA ya Usimamizi wa Sekta ya Hifadhi
ya Jamii nchini (SSRA), imewataka Watanzania kuondoa hofu iliyojengeka
kwenye jamii kuwa mifuko ya hifadhi ya jamii ina hali mbaya kifedha.
Akizungumza katika warsha maalum ya siku
moja ya waandishi wa habari, iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam,
Kaimu Mkurugenzi wa SSRA, Ansgar Mushi alisema kuwa mifuko hiyo haina
hali mbaya kama wanavyodhani watu katika jamii kwani ina fedha za
kutosha.
“Watanzania wamekuwa wakiambizana kuwa
mifuko hii ina hali mbaya kifedha, napenda kuwahakikishia kuwa ina fedha
za kutosha kwani tumekuwa tukifanya ukaguzi wa mara kwa mara. Katika
kaguzi zetu za mara kwa mara hakuna mfuko tuliobaini kuwa una kasoro au
upungufu wowote,” alisema Mushi.
Aidha, Mushi alisema kwa mwaka mifuko
hiyo ya pensheni imekuwa ikikusanya jumla ya sh trilioni 1.692 wakati
mfuko wa bima ya afya (NHIF) unakusanya sh bilioni 88.5 ambapo jumla ya
makusanyo yote ni sh trilioni 1.78.
Kwa upande wa fao la kujitoa, Mushi
alisema licha ya kutawaliwa na sintofahamu, fao hilo lilifutwa na
Serikali kuanzia mwaka 2012 na kwa sasa SSRA imeanzisha mchakato wa
kuratibu uanzishwaji wa fao la upotevu wa ajira.
Mushi alisema kuwa fao hilo lilipofutwa,
bado kulikuwa na mifuko iliyoendelea kuruhusu kujitoa lakini kwa sasa
wameamua waanzishe mchakato wa fao la kupoteza ajira, ambalo ni mahususi
kwa ajili ya kuwanufaisha waathirika.
“Fao la Upotevu wa ajira litakuwa
mahsusi kwa ajili ya wale waliopoteza ajira zao, huku wakiwa wamechangia
mifuko ya hifadhi kwa kipindi cha miezi zaidi ya 18. Hawa watalipwa
asilimia 33 ya mshahara wa mwisho kwa kipindi cha miezi 6,”
“Kipindi hicho cha miezi 6 kikiisha, mtu
huyo kama hajapata ajira atawekwa katika hatua nyingine ambapo
ataruhusiwa kuchukua nusu ya fedha alizochangia katika kipindi chake cha
ajira,” alisema Mushi.
Akizungumzia wale waliopoteza ajira zao
wakiwa hawajafikisha kipindi cha miezi 18, Mushi alisema kuwa
wataruhusiwa kuchukua asilimia 100 ya fedha walizochangia kipindi chote
walipokuwa kwenye ajira.
“Watu hao wataruhusiwa kuchukua fedha
zao kwa asilimia 100 ambazo walichangia kipindi wakiwa waajiriwa. Hata
hivyo, napenda kuwaambia Watanzania kuendelea kuichangia mifuko hiyo
kwani ina manufaa zaidi nyakati za uzeeni baada ya kustaafu,” alisema
Mushi.
SSRA YAWATOA HOFU WANANCHI KUHUSU MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII NCHINI
Reviewed by crispaseve
on
07:35
Rating:
Post a Comment