RC MONGELLA AFUNGUA MKUTANO WA ROBO MWAKA WA CHAMA CHA MAJAJI NA MAHAKIMU MIKOA MWANZA NA GEITA.
Mkuu wa Mkoa wa
Mwanza, Mhe.John Mongella, akizungumza kwenye Ufunguzi wa Mkutano wa
Robo Mwaka wa Chama cha Majaji na Mahakimu JMAT, tawi la Mwanza na
Geita, unaofanyika leo kwenye ukumbi wa jengo la NSSF Jijini Mwanza.
Mongella
amewataka wajumbe wa mkutano huo kujadili kwa uwazi masuala ya maadili
kwa watumishi wa umma na kwamba yawe ajenda ya kudumu katika ngazi
mbalimbali za utendaji serikalini hususani katika ngazi ya mahakama.
Amesisitiza
mkutano huo kutoka na maadhimio yanayohimiza mahakama kutenda haki na
kuleta manufaa kwa wananchi na kuondokana na malalamiko kwamba mahakama
hazitendi haki katika maamuzi yake.
Mwenyekiti wa
JMAT tawi la Mwanza, Francis Kishenyi, ambaye pia ni Hakimu Mkazi
Mfawidhi Wilaya ya Ukerewe mkoani Mwanza, chama hicho kinahakikisha
watumishi wa mahakama wakiwemo Majaji na Mahakimu wanafanya kazi kwa
kutenda haki na kuwafanya wananchi kutambua umuhimu wa chombo hicho
katika utoaji wa haki.
Pamoja na mambo mengine, mkutano huo unajadili masuala mbalimbali ikiwemo maadili ya viongozi wa Umma.
Na BMG
Jaji Mfawidhi Kanda ya Ziwa, Mhe.Robert Makaramba, akizungumza kwenye mkutano huo.
Mwenyekiti wa JMAT tawi la Mwanza,
Francis Kishenyi, ambaye pia ni Hakimu Mkazi Mfawidhi Wilaya ya Ukerewe
mkoani Mwanza, akizungumza na wanahabari nje ya mkutano huo.
Hakimu Mkazi Mwandamizi, Mfawidhi mkoani
Mwanza, Mhe.Wilbert Martin Chuma, akizungumza kwenye mkutano wa robo
Mwaka wa Chama cha Majaji na Mahakimu mikoa ya Mwanza na Geita,
unaofanyika leo Jijini Mwanza.
Viongozi mbalimbali wakiwa meza kuu kwenye mkutano huo
Viongozi mbalimbali wa vyombo vya Ulinzi na Usalama mkoani Mwanza, wakiwa kwenye mkutano huo.
Viongozi mbalimbali kutoka Shirika la Taifa la Hifadhi ya jamii NSSF mkoani Mwanza, wakiwa kwenye mkutano huo.
Wajumbe wa mkuatno huo
Katibu wa JMAT
ambaye pia ni Hakimu Mkazi mkoani Mwanza, Bittony Mwakisu (kulia) akiwa
pamoja na Domician Mlashani, Hakimu Mkazi Mahakama ya Mwanzo wilayani
Sengerema na mjumbe wa Kamati tendaji JMAT (kushoto).
Picha ya pamoja
Viongozi mbalimbali kwenye picha ya pamoja
Picha ya pamoja
Pamoja na mambo mengine, mkutano huo unajadili masuala mbalimbali ikiwemo maadili ya viongozi wa Umma.
RC MONGELLA AFUNGUA MKUTANO WA ROBO MWAKA WA CHAMA CHA MAJAJI NA MAHAKIMU MIKOA MWANZA NA GEITA.
Reviewed by crispaseve
on
06:38
Rating:
Post a Comment