UJUMBE KUTOKA CHAMA CHA CPC CHA CHINA WATUA NCHINI KUJIFUNZA KAZI ZA CCM
Mkutano ukiendelea.
Wajumbe hao wakisikiliza kwa makini maelezo kutoka kwa Mwenyekiti wa CCM, Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhan Madabida.
Makada wa CCM wakijumuika na wajumbe wenzao kutoka china.
Mratibu wa Masuala ya Siasa na Uhusiano
wa Kimataifa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk. Pindi Chana (kushoto),
akizungumza na wajumbe hao.
Madabida akiwakaribisha wajumbe hao.
Karibuni wajumbe kutoka China.
Na Dotto Mwaibale
UJUMBE wa watu sita kutoka Chama cha
Kikomunisti cha China (CPC) umewasili nchini kwa ziara ya siku saba
kujifunza shughuli mbalimbali zinazofanywa na Chama Cha Mapinduzi (CCM)
Akizungumza na waandishi wa habari
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam Ramadhani Madabida alisema
ujumbe huo umeongozwa na Mkurugenzi wa Idara ya Mahusiano ya Kimataifa,
Maendeleo na Mafunzo wa Chuo cha Viongozi wa chama hicho, Jia Bo.
Madabida alisema ziara ya ujumbe huo
hapa nchini ni kudumisha ushirikiano baina ya Tanzania na China
ulioasisiwa na Hayati Baba wa Taifa na kiongozi wa Taifa hilo Hayati Mao
Tse-Tung.
Alisema ujumbe huo ambao utatembelea
Wilaya ya Temeke na Zanzibar umewasili nchini kufuatia ziara ya baadhi
ya makada wa CCM walipokwenda nchini China ambapo walijifunza mambo
mbalimbali ambayo ujumbe huo utapenda kujua kama wameyafanyia kazi.
Mratibu wa Masuala ya Siasa na Uhusiano
wa Kimataifa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk. Pindi Chana alisema ujio
wa viongozi wa chama hicho kutoka China ni matunda ya ushirikiano wa
Tanzania na nchi mbalimbali duniani.
" Ujio wa wenzetu hawa kutoka China ni
matunda ya ushirikiano kati yetu na nchi nyingine kama Zimbabwe, Afrika
Kusini, Angola, Cuba, Ulaya hasa katika siasa za kijamaa" alisema
Chana.
Alisema wenzetu wa China wapo karibu
bilioni moja na wamepiga hatua katika maeneo mbalimbali hivyo ujio wao
hapa nchini ni fursa kwao kujifunza mambo yetu na sisi kujifunza kwao
kutokana na hatua ya kiuchumi waliyonayo.
UJUMBE KUTOKA CHAMA CHA CPC CHA CHINA WATUA NCHINI KUJIFUNZA KAZI ZA CCM
Reviewed by crispaseve
on
22:19
Rating:
Post a Comment