WATANZANIA WATAKIWA KUCHANGAMKIA 'BLACK FRIDAY

Na Dotto Mwaibale
TUNAPOELEKEA mwisho wa mwaka wa 2016
huku sikukuu za krisimasi na Mwaka Mpya zikiwa zinakaribia, Watanzania
wametakiwa kuchangamkia ofa za ‘Black Friday’ inayolenga kupunguza
pakubwa bei ya kukaa kwenye hoteli nchini.
Rai hiyo imetolewa na kampuni inayotoa
huduma za hoteli mtandaoni ya Jumia Travel ambapo inamuwezesha mtu
kujionea hoteli mbalimbali, upatikanaji wa huduma, bei, mahali zilipo na
pia fursa ya kuweza kulipia kabisa.
Mtandao huo umeingia makubaliano na
hoteli kadhaa za Tanzania bara na visiwani Zanzibar katika kuhakikisha
wateja wanaonja utamu wa huduma zao kwa punguzo kubwa ambalo limekuwa
likiendelea kwa wiki mbili sasa na litafikia kilele mnamo Ijumaa tarehe
25 Novemba mwaka huu.
Akifafanua zaidi kuhusu siku hii ya
Black Friday, Meneja Mkaazi wa Jumia Travel Tanzania Bi. Fatema Dharsee
amesema kuwa hoteli ambazo zimetoa ofa hiyo ni pamoja na Africa House na
Jaffreji House & Spa zilizoko katika Kisiwani Zanzibar pamoja na
White Sands na Landmark Beach Resort & Conference Center zilizopo
Tanzania Bara.
“Ninafahamu kuwa wengi wetu huwa
tunatamani kutumia muda huu wa mapumziko katika sehemu nzuri yenye
starehe zote tofauti na mazingira tuliyoyazoea. Hilo linawezakana kwani
kupitia ushirikiano na hoteli tunazofanyakazi nazo tunawatangazia ofa ya
punguzo kubwa la kwenda kujivinjari katika hoteli za nyota nne ambayo
imeanza wiki iliyopita Novemba 14 na itadumu mpaka Novemba 25,”
alifafanua.
“Kupitia ofa hii unaweza kuitumia pamoja
na mpendwa wako, familia, ndugu, jamaa au marafiki. Kwa mfano, White
Sands wanayo michezo ya kwenye maji, kituo cha kupiga mbizi chini ya
maji na safari ya boti kwenda kisiwani. Tunawasihi watanzania kutumia
fursa kama hizi ili kuweza kujionea huduma nzuri na hadhi ilizonazo
hoteli za hapa nyumbani. Itakuwa ni jambo zuri sisi kwanza kuwa mabalozi
wa vitu vyetu wenyewe na sio wageni wanaokuja kutembelea nchini.”
Alimalizia Meneja huyo Mkazi wa Jumia Travel Tanzania
Kutokana na maendeleo ya teknolojia
Jumia Travel (travel.jumia.com) inamuwezesha mteja kufanya huduma zote
za hoteli kupitia programu inayoweza kupatikana kwenye kompyuta, tabiti
na simu. Hivyo basi kurahisisha upatikanaji wa huduma kwa njia rahisi na
uhakika bila ya kumlazimu mtu mpaka kutembelea hoteli anayoitaka moja
kwa moja.
Kuhusu Jumia Travel
Jumia Travel (travel.jumia.com) ni
kampuni nambari moja unaongoza wa huduma za hoteli kwa njia ya mtandao
barani Afrika ambao humruhusu mteja kupata bei nzuri za hoteli zaidi ya
25,000 kwa nchi za Afrika na zaidi ya hoteli 200,000 duniani kote.
Dhumuni letu ni kuleta kila aina ya
huduma za malazi kwenye mfumo wa mtandao na kutengeneza njia rahisi na
nafuu zaidi kwa wateja kuzilipia.
Hapa Jumia Travel, tunao mamia ya
wataalamu katika masuala ya utalii ambao huwasiliana na wateja wetu.
Ofisi zetu zinapatikana katika miji na nchi zifuatazo Lagos (Naijeria),
Accra (Ghana), Dakar (Senegali), Abidjan (Ivory Coast), Algiers
(Algeria), Douala (Cameroon), Kampala (Uganda), Dar es Salaam
(Tanzania), Nairobi (Kenya), Addis Ababa (Ethiopia), Porto (Ureno) na
Paris (Ufaransa).
Kabla ya mwezi Juni 2016, Jumia Travel
ilikuwa ikijulikana kama Jovago. Ilianzishwa mnamo mwaka 2013 na Jumia
huku ikiendeshwa kwa ushirikiano wa karibu na makampuni kama vile MTN,
Rocket Internet, Millicom, Orange na Axa.
WATANZANIA WATAKIWA KUCHANGAMKIA 'BLACK FRIDAY
Reviewed by crispaseve
on
04:23
Rating:
Reviewed by crispaseve
on
04:23
Rating:

Post a Comment