SERIKALI YAOMBWA KUWAPATIA BIMA YA AFYA WALEMAVU WA NGOZI
Na Anthony John Globu ya Jamii.
CHAMA cha watu wenye ualbino Tanzania (TAS) kimetoa wito kwa
Serikali kuwapatia bima ya Afya watu wenye ulemavu wa ngozi ili kuweza
kuwasaidia pale wanapokuwa na matatizo ya kiafya.
Akiongea na waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam katika
Ofisi ya chama hicho iliyopo hospitali ya Ocean Road, Muweka hazina
Abdilah Omary amesema watu wenye ualbino hasa waliopo vijijini wanapata
changamoto kubwa ya upatikanaji wa matibabu hasa pale wanapo sumbuliwa
na magonjwa mbali mbali.
Abdilah ametoa wito kwa jamii na familia zenye watu wenye ualbino
kuwapa malezi yanayoendana na hali yao tofauti na Jamii nyingi kwa hivi
sasa wanawalazimisha watu wenye ualbino kufanya kazi ngumu kama
kuchunga ngo'mbe na kulima.
Wakati huo huo wajumbe wa chama cha watu wenye ualbino Tanzania
wamemchangia kiasi cha sh.milioni moja Leonard Gaspar mwenye ulemavu wa
ngozi Mkazi wa Morogoro Matombo anayesumbuliwa na kansa ya ngozi.
Hata hivyo Leonard amewashukuru wajumbe wa chama hicho kwa
mchango huo huku akiomba jamii na wadau mbalimbali kuwapa msaada pale
wanapoweza ili apate mtaji wakumsaidia katika maisha ya kila siku na
matibabu.
Chama hicho cha watu wenye ualbino Tanzania wametoa wito kwa jamii
kumsaidia kijana Leonard anaye sumbuliwa na tatizo la kansa ya ngozi
kwa muda mrefu.
Hata Hivyo Abdilah ameomba Jamii ya watanzania watakaoguswa na
tatizo alilonalo Leonard wanaweza kutoa michango yao kwa kuwasiliana na
Ofisi za Chama Cha Watu Wenye Ualbino kilichopo Katika Hospital ya Ocean
Road.
Muweka
hazina wa Chama cha Watu wenye Ualbino Tanzania, Abdilah Omari akiwa
pamoja Leonard Gasper anayesumbuliwa na tatizo la kansa na kumpatia
msaada wa kiasi cha fedha milioni moja kwa ajili ya matibabu.
SERIKALI YAOMBWA KUWAPATIA BIMA YA AFYA WALEMAVU WA NGOZI
Reviewed by crispaseve
on
06:07
Rating:
Post a Comment