SHIRIKA LA NDEGE LA ETIHAD LA SHEREHEKEA MWAKA MMOJA WA MAFANIKIO YAKE TANZANIA.
Shirika
la Ndege la Etihad lenye makao makuu yake nchi za falme za kiarabu,
limetimiza mwaka mmoja wa mafanikio tangu lianze kufanya huduma zake
nchini Tanzania ikiwamo kuleta mabadiliko makubwa kwenye biashara ya
usafiri wa anga kwa wasafiri wa Dar es Salaam na makao makuu ya falme
hizo, Abu Dhabi.
Zaidi
ya wasafiri 60,000 wametumia usafiri huo tangu kuzinduliwa kwa huduma
zake ambazo zinawaunganisha abiria wengi na miji mikubwa duniani, tangu
Desemba Mosi 2015. Wasafiri wengi wamekuwa wakitumia usafiri wa Shirika
la ndege la Etihad kutokana na shirika hilo kuwa kitovu cha safari za
kwenda Ulaya na Asia.
Shirika
hilo linatoa huduma zake kwa kutumia ndege mbili za Airbus A320 yenye
nafasi 16 kwa daraja la kwanza na viti 120 kwa daraja la kawaida. Kwa
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Dar es
Salaam,ndiyo ndege ya tatu kuondoka kutoka Afrika Mashariki ikipitia
Uwanja wa Ndege wa Nairobi Kenya na Entebbe Uganda.
Meneja
Mkuu wa Kanda ya kusini mwa jangwa la Sahara wa Shirika la Ndege la
Etihad, John Friel alisema, " Kwa mwaka mmoja tangu kuanza kwa huduma
zetu kumekuwa na mafanikio makubwa, ndiyo sababu tuliamua kuichagua
Tanzania kwa ajuili ya kufanya shughuli zetu. Tunafurahia kufanya kazi
kwa ufanisi jambo ambalo limewavutia wateja wengi kulingana na mahitaji
ya soko la usafiri wa anga hapa nchini."
"Lengo
letu ni kuendelea kushirikiana na wadauwa sekta hii ya anga hapa nchini
ili kuhakikisha kwamba abiria wengi zaidi wanatumia usafiri wetu ambao
umepata heshima kubwa ulimwenguni kwa kunyakua tuzo mbalimbali za ubora
zinazotolewa na Shirika la Ndege la Etihad,” alisema.
SHIRIKA LA NDEGE LA ETIHAD LA SHEREHEKEA MWAKA MMOJA WA MAFANIKIO YAKE TANZANIA.
Reviewed by crispaseve
on
03:50
Rating:
Post a Comment