Header AD

UWANJA WA NDEGE WA MWANZA KUKAMILIKA NOVEMBA.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa Mhandisi Lili-Ang kutoka kampuni ya Beijing Construction Engineering Group (BCEG) inayakarabati na kujenga uwanja wa ndege wa Mwanza.
Mhandisi Mshauri anayesimamia ukarabati na ujenzi wa uwanja wa ndege wa Mwanza akimuonesha Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa Mnara wa jengo la kuongozea ndege alipokagua ujenzi wa uwanja huo.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa viongozi wa uwanja wa ndege wa Mwanza namna ya kushirikiana na Mkandarasi Beijing Construction Engineering Group (BCEG) anayekarabati na kujenga uwanja huo.
Muonekano wa jengo jipya la kuongozea ndege linalojengwa na kampuni ya Beijing Construction Engineering Group (BCEG) katika uwanja wa ndege wa Mwanza.

…………

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amemtaka Mkandarasi anayejenga na kukarabati uwanja wa ndege wa Mwanza Beijing Construction Engineering Group (BCEG), kuhakikisha ujenzi huo unakamilika ifikapo Novemba mwaka huu.

Akizungumza mara baada ya kukagua ujenzi wa mnara wa kuongozea ndege, jengo la kuhifadhia mizigo, eneo la kuegeshea ndege na jengo la umeme litakalotoa huduma katika uwanja huo, Profesa Mbarawa amesema tayari Serikali imeshamlipa mkandarasi huyo kiasi cha shilingi bilioni saba kwa ajili ya ujenzi huo.

“Sisi tumeshamlipa pesa yake yote na hivyo tunachotaka kwake ni kukakamilisha kazi yetu kwa wakati ili kuupa hadhi inayostahili uwanja wa ndege wa Mwanza amboa ni kiungo muhimu katika kanda ya Ziwa”, Amesema Profesa Mbarawa.

Prof. Mbarawa amemuagiza Meneja wa uwanja wa ndege wa Mwanza Bi .Easter Madale kuhakikisha vikwazo vyote vinavyomkabili mkandarasi vinaondolewa ili kumuwezesha kufanya kazi kubwa kabla ya kipindi cha mvua za masika zinazotarajiwa kuanza mwezi machi.

Kwa upande wake Mhandisi Lili Ang aneyesimamia ujenzi huo kutoka kampuni ya BCEG amemhakikishia Prof. Mbarawa kuwa baada ya kupokea malipo wamejipanga kukamilisha kazi hiyo kwa wakati na viwango ili waweze kupata fursa nyingine za ujenzi hapa nchini.

Naye Meneja wa Uwanja wa ndege wa Mwanza Bi .Easter Madale ameyataka mashirika ya ndege kuongeza safari za ndege kwenye uwanja wa Mwanza kwa kuwa sasa utakuwa na hadhi ya kimataifa na kusisitiza umuhimu wa wawekezaji wa hoteli, vituo vya mafuta na maduka makubwa kuwekeza karibu na uwanja huo ambao ndio lango la uchumi wa kanda ya ziwa.

Katika hatua nyingine Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano ameelekea mkoani Simiyu kuanza ziara ya siku mbili mkoani humo amabapo pamoja na mambo mengine anatarajiwa kushiriki katika ufunguzi wa barabara ya Bariadi- Lamadi iliyojengwa kwa kiwango cha lami.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawssiliano
UWANJA WA NDEGE WA MWANZA KUKAMILIKA NOVEMBA. UWANJA WA NDEGE WA MWANZA KUKAMILIKA NOVEMBA. Reviewed by crispaseve on 00:41 Rating: 5

No comments

Post AD