DC SHINYANGA AKABIDHI VIFAA TIBA VILIVYOTOLEWA NA WATANZANIA WAISHIO DENMARK KWA AJILI YA WANANCHI WA SHINYANGA
Hapa ni katika viwanja vya Ofisi ya
Mtendaji Kata ya Ngokolo katika manispaa ya Shinyanga ambapo leo
Jumamosi Februari 11,2017 Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro
amekabidhi vifaa tiba kwa mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga kwa ajili
ya kuvisambaza katika zanahati na hospitali zilizopo katika manispaa
hiyo.
Vifaa tiba hivyo vimetolewa na Watanzania waishi nchini Denmark ambapo
upatikanaji wa vifaa hivyo unatokana ushirikiano wa Diwani wa kata ya
Ngokolo Emmanuel Ntobi (CHADEMA) na shirika la AGAPE la Mjini Shinyanga
kuwasiliana Watanzania waishio nchini Denmark kisha kuleta vifaa hivyo.
Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo,Mkurugenzi wa shirika la AGPAE
John Myola alisema wazo la kutafuta vifaa tiba lilitolewa na diwani wa
kata ya Ngokolo Diwani Emmanuel Ntobi ambaye anajuana na watanzania
waishio nchini Denmark.
“Diwani huyu alitupatia mawasiliano ya watu hao wanaojulikana Denish
Relief Group kisha sisi kama shiriki tukaandika andiko tukiomba kupewa
vifaa tiba kwa ajili ya kupunguza uhaba wa vifaa tiba katika zahanati na
hospitali za manispaa ya Shinyanga”,alisema Myola.
Myola alitumia fursa hiyo kuiomba ofisi ya mkurugenzi wa manispaa ya
Shinyanga kuhakikisha kuwa vifaa tiba hivyo vinatumika kama inavyotakiwa
na kuhakikisha vinatunzwa.
Naye Diwani wa kata ya Ngokolo Emmanuel Ntobi alisema watanzania waishio
Denmark wametoa vifaa tiba hivyo bure kwa ajili ya watanzania huku
akiishukuru serikali kuruhusu vifaa hivyo kuingia nchini bila kulipiwa
kodi.
“Hili jambo la kidiplomasia kwa nchi hizi mbili Tanzaia na
Denmark,Denish Relief Group ni kundi la watu la kwanza kutoa msaada
mkubwa nchini,huu ni kama mwanzo tu,wamesema wataendelea kutoa msaada na
wamesema wapo tayari kutujengea zahanati katika kata hii ya Ngokolo
ambayo haina zahanati”,alisema Ntobi.
“Tumepokea vifaa tiba aina 26,vimo vitanda,magodoro,viti vya kisasa vya
wagonjwa,mashine ya Utra sound,mashine ya Incubation na vifaa vingine
vingi ambavyo vitatumika katika kutoa huduma za afya kwa wananchi wa
manispaa ya Shinyanga”,aliongeza Ntobi.
Hata hivyo diwani huyo aliomba vifaa hivyo vitumike vizuri na vitumike kwa wananchi wenye kipato cha hali ya chini.
Alisema pamoja na kutoa vifaa tiba,pia watanzania hao waishio nchini
Denmark wametoa baiskeli kwa watu wenye ulemavu na nguo kwa makundi ya
watu wasiojiweza wakiwemo wazee wanaolelewa katika kituo cha Kolandoto
kilichopo katika manispaa ya Shinyanga.
Kwa upande wake mgeni rasmi katika makabidhiano hayo,Mkuu wa wilaya ya
Shinyanga Josephine Matiro alipongeza jitihada zilizofanywa na shirika
la AGAPE na diwani wa kata ya Ngokolo katika kupatikana kwa vifaa
hivyo.
“Hili ni tukio kubwa na la busara sana,limetutia moyo ,nawapongeza sana
watanzania waishio Denmark na wote mliofanikisha kupatikana kwa vifaa
hivi ambavyo vitakuwa msaada mkubwa kwa wananchi,huu siyo muda wa
kufanya siasa,kinachotakiwa ni kuwaletea maendeleo wananchi bila kujali
itikadi za kichama”,alieleza Matiro.
“Katika suala la maendeleo,serikali ipo tayari kushirikiana na
shirika,kundi lolote la watu na hata mtu binafsi,tusitumie majukwaa ya
maendeleo kufanya siasa,nimpongeze diwani wa kata hii kwa ushirikiano
aliotuonesha katika kuwasaidia wananchi”,aliongeza Matiro.
Mwandishi mkuu wa Malunde1 blog,Kadama
Malunde alikuwepo wakati wa makabidhiano hayo ametuletea picha 30 za
matukio..Tazama hapa chini
Vifaa tiba vilivyotolewa na watanzania waishio nchini Denmark kwa ajili
ya kusaidia kutoa huduma za afya katika zahanati na hospitali zilizopo
katika manispaa ya Shinyanga
Vifaa vya kufanyia mazoezi na viti vya kubebea wagonjwa
Vifaa tiba mbalimbali ikiwemo magongo,viti vya kuogea
Vifaa tiba vikiwa katika viwanja vya ofisi ya Afisa mtendaji kata ya Ngokolo katika manispaa ya Shinyanga
Baiskeli za wagonjwa na vifaa tiba vingine vya kisasa
Vitanda vya wagonjwa
Vitanda vikiwa na magodoro yake
Afisa Mtendaji wa kata ya Ngokolo William Ndila akitambulisha wageni
mbalimbali waliohudhuria hafla fupi ya kukabidhi vifaa tiba
vilivyotolewa na watanzania waishio nchini Denmark "Denish Relief Group"
kutokana na jitihada zilizofanywa na diwani wa kata hiyo Emmanuel Ntobi
na Shirika la AGAPE
Mkurugenzi wa shirika la AGAPE la Mjini Shinyanga John Myola akizungumza katika hafla hiyo
Wananchi wakiwa eneo la tukio
Aliyesimama ni Mkurugenzi wa shirika la AGAPE la Mjini Shinyanga John
Myola akielezea namna vifaa tiba vilipatikana kwa ajili ya kusaidia
kutoa huduma za afya kwa wananchi wa manispaa ya Shinyanga
Diwani wa kata ya Ngokolo katika manispaa ya Shinyanga Emmanuel
Ntobi(Chadema) akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa tiba
hivyo.Kushoto ni diwani wa viti maalum Zainab Heri (Chadema).Kulia ni
mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro
Wananchi wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea
Diwani wa kata ya Ngokolo katika manispaa ya Shinyanga Emmanuel
Ntobi(Chadema) aliwashukuru viongozi wa serikali kwa kuruhusu vifaa tiba
hivyo kuingia nchini bila kodi huku akiomba serikali kuwapatia eneo kwa
ajili ya kujenga zahanati katika kata hiyo ambayo haina zahanati
kutokana na kushindwa kujenga baada ya kuibuka mgogoro kwenye eneo
ambapo kulitakiwa pajenge zahanati
Kaimu Mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga Magendi Magenzi ambaye ni
afisa utumishi wa manispaa hiyo,akizungumza katika hafla hiyo ambapo kwa
namna ya pekee alimpongeza diwani wa kata ya Ngokolo kwa jitihada
alizofanya katika upatikanaji wa vifaa tiba hivyo.
Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Ngokolo John Nangi akizungumza wakati wa hafla hiyo
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza wakati wa hafla
hiyo ambapo alisema serikali inaunga mkono jitihada zinazofanywa na
wadau mbalimbali katika kuwaletea maendeleo wananchi
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza katika hafla hiyo
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akisisitiza umuhimu wa kuendeleza siasa kwenye masuala ya maendeleo
Diwani wa kata ya Ngokolo Emmanuel Ntobi akimwonesha mkuu wa wilaya
vifaa tiba hivyo ikiwemo vifaa vya kubebea watoto na vifaa vya kufanyia
mazoezi
Diwani wa kata ya Ngokolo Emmanuel Ntobi akiendelea kumwonesha mkuu wa
wilaya ya Shinyanga vifaa tiba,pichani ni meza za kulia chakula na
kabati
Diwani wa kata ya Ngokolo Emmanuel Ntobi akionesha vifaa tiba
Diwani wa kata ya Ngokolo Emmanuel Ntobi akiwa ameshikilia fimbo za watu wasioona
Baada ya kukabidhi baiskeli kwa ajili ya watu wenye ulemavu wa
viungo,Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akishikana mkono na
Richard ambaye ni mlemavu wa viungo.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akisalimiana na kijana mwenye ulemavu wa viungo baada ya kumkabidhi baiskeli
Wananchi wenye ulemavu wa viungo wakiwa wamekaa kwenye baiskeli
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro na mkurugenzi wa shirika la
AGAPE John Myola wakiwasindikiza wananchi wenye ulemavu wa viungo baada
ya kuwapatia baiskeli hizo.Baiskeli hizo zinaendelea kutolewa kwa
wananchi mbalimbali wenye ulemavu wa viungo
Mashine ya Utra Sound ambayo pia imetolewa na watanzania waishio Denmark
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza baada ya kuona
mashine mbili Utra Sound kwa ajili ya akina mama wajawazito na Mashine
ya kukuzia watoto njiti
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza baada ya kuona mashine za kisasa za kutolea huduma za afya
Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog
DC SHINYANGA AKABIDHI VIFAA TIBA VILIVYOTOLEWA NA WATANZANIA WAISHIO DENMARK KWA AJILI YA WANANCHI WA SHINYANGA
Reviewed by crispaseve
on
08:10
Rating:
Post a Comment